Nov 9, 2017
Umezaliwa Ili Kufanya Mambo Haya Tu…
Kila siku iitwapo leo, yapo
mambo makubwa yanayokamilishwa ikiwemo
ndoto na mipango na watu wenye sifa kama za kwako.
Tunaona viwanda vikubwa,
miradi mikubwa inagunduliwa na watu wenye changamoto na wanaoishi mazingira
kama yale yale uliyonao wewe.
Pia hata ukiangalia
mabadiliko ya kisayasansi yanayotokea kila siku na kuubadilisha ulimwengu, yanasababishwa
pia na watu wale wale wenye sifa kama za kwako.
Mpaka hapo unaona hiyo yote
inadhihirisha au inakuhakikishia kwamba, binadamu umezaliwa kwa kusudi moja tu
la kufanya mambo makubwa.
Kama ulikuwa umefika mahali
unajidharau na kujiona wewe kama ni panzi utakuwa unakosea sana, hujazaliwa uwe
hivyo hata kidogo.
Umezaliwa kuweza kufanya
mapinduzi makubwa sana kwenye maisha yako na maisha ya wengine pia.
Unatakiwa kuujua uwezo
mkubwa uliondani mwako. Kwa kuujua uwezo huo ulio ndan mwako inakusaidia sana
kuleta mabadiliko ya kweli na makubwa.
Kwa sasa tunaishi katika
dunia ambayo ina uwezo wa kutupa mabadiliko na mafanikio yoyote tunayatakayo.
Usiangalie hali ya kipato
chako au maisha yako yalivyo kwa sasa, unachatakiwa kujua kwamba unaweza kufanya
mabadikilo makubwa sana na ya kushangaza.
Umezaliwa kufanya makubwa
hapa duniani. Kama kila wakati umekuwa ukiwazia kufanya mipango midogo midogo
hiyo sio saizi yako.
Unachotakiwa kufanya ni
kubadilisha msimamo wako mara moja na kuelekea upande mwingine wa kufanya
makubwa.
Kufanya yaliyo makubwa kwenye
maisha yako, hakutokani na pesa ni
matokeao ya kuamua kwanza na kujua ni wapi unakotaka kufika.kimaisha.
Unayo nafasi ya kufanya maisha
yako ya hapa duniani yakawa bora kama wewe unavyotaka yawe. Hakuna mtu wa
kukuzuia katika hilo.
Muda wa kuanza kufanya yale
yaliyo makubwa katika maisha yako ni sasa. Hutakiwi kusubiri kesho au lini, huu
ndio muda wako.
Ipo miradi mikubwa sana
ambayo inakusubiri wewe uikamilishe. Ikiwa utacheza hutaweza kufanikisha kitu
chochote.
Msisitizo ninaotaka ujue
hapa katika makala haya ni kwamba, wewe umezaliwa kwa kufanya mambo makubwa na
sio kinyume chake.
Kwa hiyo asikudanganye mtu
eti huwezi au wewe ni mdogo sana, unayo nafasi ya kuweza kufika mbali
kimafanikio kwa kufanya yaliyo makubwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.