google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 2, 2017

Kama Utakosa Mambo Haya Mawili, Mafanikio Basi Tena.

No comments :
Kuaminiwa kwa jambo lolote lile, kunatokana na ukweli. Hata kama ukweli huo unauma sana, lakini chanzo cha kuaminiwa ndiko kinapoanzia huko.
Hautaweza kuamiiwa na mtu yeyote kama ndani yako huna alama za ukweli ambazo zinaonekana, zaidi utazidi kuonekana ni wa kawaida na mwongo.
Na bila kuaminiwa pia, hakuna kitu ambacho utaweza kukifanikisha sana. Hiyo yote ni kwa sababu mafanikio mara nyingi yanaanza kujengwa na kuaminiwa.
Ukiweza kuaminiwa hata ukiwa huna mtaji unaweza ukafanya biashara, lakini kosa kubwa linakuja hasa pale unaposhindwa kwa mwaminifu, hakuna atayekuhitaji.

Kwa hiyo unaona uamifu pekee ni kama mtaji, lakini uaminifu hauanzi hivi hivi tu, lazima kwanza ukweli ndani yako uwepo. 
Ili uweze kuaminika unatakiwa uelewe hata unapofanya kazi na wengine unatakiwa uwe mkweli sana kutoka kwenye kauli zako na mengineyo mengi.
Bila uaminifu kuwepo kwenye maisha ya kawaida basi mambo mengi ni yatakwama sana. na zipo huduma zitakufa kabisa.
Unaona mpaka hapo unatakiwa kujenga uaminifu mkubwa sana kwenye kila ukifanyacho ili kikupe mfanikio, lakini sehemu ya kuanzia ni kwenye ukweli.
Je, wewe ni mkweli kiasi gani na kwa akina nani, hapo ndipo nguzo ya kuaminiwa inapoanzia na watu wengi wakakubali.
Hakuna mtu ambaye yupo duniani hapa anaaminiwa lakini asiwe mkweli, ukweli ni kitu ambacho kinasaidia sana kujenga uaminifu.
Hivyo  unaona bila ukweli hakuna uaminifu wowote. Hiyo inadhihirisha kabisa bila mambo haya mawili hakuna mafanikio ya kweli.
Mafanikio ya kweli na kwa wengine yanaanza kwa wewe kuwa mwaminfu na pia uaminifu huo utakusaidia tu kuweza kupata kile unachokitaka.
Unachotakiwa kufanya hapa, ni kuamua kutengeneza uaminifu wako kwa kuama kuwa mkweli kwa kila unachokifanya.
Kwa kujenga uaminifu, ndivyo utajikuta ukizidi kuyafikia mafanikio yako kila kukicha. Anza leo kuwa mwaminifu na utafika mbali sana kimafanikio.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.