Nov 16, 2017
Maisha Yako Yanajengwa Sana Na Mambo Haya Matatu.
Yapo
mambo mengi ambayo yanajenga maisha yako au yanafanya maisha yako yawe kama
hivyo yalivyo. Lakini hata hivyo pamoja na mambo hayo mengi, yapo mambo matatu
ya msingi ambayo yanajenga maisha yako au ndio msingi wa maisha yako.
Kama
utapuuzia ama hautaweza kujali mambo hayo matatu tu, basi kufanikiwa kwako kutakuwa
ni kitu ambacho hakiwezekani. Mimi na wewe tunatengeneza mafanikio au kushindwa
kwetu kupitia mambo hayo.
Sina
shaka, una hamu ya kutaka kujua ni mambo gani ambayo yanapelekea maisha yako
kujengwa. Sasa kamata kalamu na karatasi, kisha twende pamoja kwenye darasa
kuweza kujifunza somo letu la leo.
Jambo la kwanza, mawazo yako.
Kila
kitu unachokitaka kinaanzia kwenye mawazo yako. Hakuna jambo ambalo lipo
duniani limeanzia nje ya mawazo. Mawazo yana mchango mkubwa katika kukupa chochote
ukitakacho kwenye maisha yako.
Ukishindwa
katika mawazo yako, na nje utashindwa pia. Ndio maana ili kufanikiwa unatakiwa
kila wakati uwe na mawazo chanya sana, mawazo yakujenga, mawazo ambayo
yatakutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine.
Na
mawazo haya hayawezi kuja kwa bahati mabya tu, mawazo haya yanakuja kwa wewe
kujilisha vitu chanya karibu kila siku. Unatakiwa ujifunze vitu chanya, unatakiwa
uwe na marafiki chanya ambao watakusaidia kuwa na mawazo bora.
Kuendelea
kuwa na mawazo yale yale ambayo yamekuweka hapo ulipo, ni sawa na kuchagua
kupotea kwenye maisha yako. Kila siku hakikisha una mawazo bora yatakayoweza
kukusaidia wewe kufanikiwa na si kukuangusha.
Jambo la pili, vitendo vyako.
Mawazo
bora peke yake hata yawe mazuri vipi hayawezi kukusaidia kitu au hayawezi
kukufikisha mbali. Kitu kingine ambacho kinajenga maisha yako kwa sehemu kubwa
ni hatua unazozichukua kila siku.
Inatakiwa
ujiulize hatua unazochukua kila siku hata kama ni kidogo sana lakini katika
kuelekea ndoto zako ni zipi? Kama hakuna hatua unazochukua basi ujue sio
unajenga maisha yako bali ndio unayaharibu kabisa na kuwa maisha ya hovyo.
Hakuna
mafanikio ya kukaa tu, hakuna mafanikio ya kuyaongelea mdomoni, mafanikio yanajengwa
kwa kuchukua hatua. Ukiona hakuna hatua unazochukua usijidanganye kwamba
unatafuta na wewe mafanikio, maana wewe utakwama hata iweje.
Watu
wanaochukua hatua karibu kila siku, watu hao ndio wanaofanikiwa na kujenga
bahati kubwa katika maisha yao. Kwa hiyo unaona, vitendo ni kitu kimojawapo ambacho
kina mchango mkubwa sana pia katika kujenga maisha yako.
Jambo la tatu, maneno yako.
Pamoja
na kwamba una mawazo mawazo mazuri na una vitendo vizuri, lakini unatakiwa
kukumbuka maneno yako pia yanamchango mkubwa sana katika kujenga maisha yako na
yakaonekana kama hivyo yalivyo hapo.
Maisha
ya wengi yamejengwa au kuharibiwa kutokana na maneno yao waliojinenea siku za
nyuma. Ndio maana kabla hujaongea inabidi ujiulize unaongea kitu gani na je
kitu hicho kinamchango upi katika kuelekea ndoto zako.
Unaweza
ukawa mtabiri wa maisha yako, eidha kwa kwa kubomoa au kuyaumba. Maneno yako yanaumba
sana maisha yako kwa sehemu kubwa. Ukijinenea vibaya, uelewe kabisa ndivyo
maisha yako yataharibika kabisa.
Hivyo
ni muhimu kuwa na uchaguzi wa maneno bora ili ikusaidie kuweza kufanikia. Usiwe
mtabiri wa kuharibu maisha yako kila wakati. Jifunze kuwa mtabiri wa kuweza
kukusaidia kujenga maisha yako.
Kwa
kifupi, hayo ndiyo mambo makubwa matatu ambayo yanajenga maisha yako sana, ingawa
ukienda kinyume na hapo ndivyo unaharibu maisha yako kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.