Nov 27, 2017
Maskini Na Tajiri Wanatofautiana Kwa Mambo Haya…
Kila
kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano
mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika
kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na
mingine midogo ya kawaida.
Pia hata
wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na
nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua.
Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge
wanyonge.
Halikadhalika
linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na
maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna
binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa
hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu.
Kama
mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe
na matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya
wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo mambo mengi kidogo yanayosababisha wengine wawe
matajiri na wengine kuwa maskini.
Lakini
katika makala haya tutaongelea kipengele kidogo cha tabia na jinsi zinavyoleta
utofauti kati ya maskini na tajiri. Ni kweli zipo tabia ambazo matajiri wanazo
na huwafanya wao kuwa matajiri kila kukicha. Ni tabia ambazo huwatenga kabisa
na maskini na kuwaacha matajiri waendelee kufanikiwa.
Ikiwa
utaamua kujifunza na kuzifatilia tabia hizi kwa karibu, uwe na uhakika utajiri
utakuwa mikononi mwako muda sio mrefu. Nasema hivyo nikiwa na maana hii,
ukitaka kuwa tajiri fanya yale ambayo matajiri wanafanya nawe utafanikiwa.
Hebu
kwa pamoja bila kupoteza muda, tuangazie nukta kadhaa, zinazoweza kutuonyesha
tabia zinazowatenga kati ya matajiri na
maskini.
1. Kuwekeza.
Watu
wenye sifa ya utajiri ndani mwao hata kama bado hawajafika huko kwenye utajiri
halisi ni wawekezaji wazuri sana. Si watu wa kuridhika na chanzo kimoja cha
mapato. Wana vitega uchumi vingi sana ambavyo vinawasaidia kuingiza mapato kwa
wingi hata kama wamelala.
Kwa
mfano uatakuta wamewekeza kwenye mashamba, mafuta, migodi na maeneo mengine
mengi. Hii ni sifa mojawapo kubwa inawatenga maskini na matajiri. Ukiona una
kitega uchumi kimoja ujue unajizibia nafasi mwenyewe ya kuelekea kwenye utajiri
mkubwa.
2. Kuweka akiba.
Suala
la kuweka akiba kwa watu matajiri sio suala la hiari, kwao ni lazima. Angalau
huweka asilimia kumi ya kile wanachokipata. Wanajua vizuri akiba hizo ni msaada
mkubwa kwa baadae katika suala zima la kuwekeza. Wao katika kuweka akiba ni
lazima, na pia hawana mchezo katika hilo.
Kutona
na tabia hii, huwafanya wazidi kufanikiwa kila siku na kuwaacha maskini
wakibaki kuwa maskini. Ni kitu ambacho unatakiwa kujifunza na kuelewa kwamba,
akiba ni jambo la msingi sana kujiwekea kama unataka kuwa tajiri. Vinginevyo
acha kuweka akiba, uendelee kubaki kwenye umaskini.
3. Kutoa.
Tabia
nyingine inayowatenga watu matajiri na maskini ni ile hali ya kutoa. Watu
matajiri ni watoaji wazuri sana wa pesa na mali zao. Hufanya hivi si kwa sababu
wanazo nyingi, bali kutoa ni moja ya kanuni kubwa ya mafanikio walioamua
kuitumia. Huwezi kufanikiwa sana kama hutoi.
Ieleweke
hivi, maskini wanaendelea kubaki kuwa
maskini kwa sababu ya uchoyo walionao. Hukumbatia sana walivyonavyo na
kusahau kutoa. Kosa hilo huwafanya wazidi kuendelea kuwa maskini siku zote za
maisha yao. Ili kuwa tajiri ni lazima kutoa.
Kumbuka,
tabia ya kuwekeza, kuweka akiba na kutoa ni moja ya tabia kubwa zinazo watenga
matajiri na maskini. Matajiri wanajikuta wakiwa ni watu wakuzifanyia kazi tabia
hizo na kuwafanya kuwa matajiri na maskini hubaki na umaskini wao kwa sababu ya
kutokuzifanyia kazi tabia hizo. Chukua hatua ya kutenda ili kubadili maisha
yako.
Ansante
kwa kunifatilia na pia endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.