Nov 11, 2017
Jinsi Ya Kuifanya Siku Yako Iwe Ya Mafanikio Na Hamasa Kubwa Sana.
Yapo
mambo ya wazi ambayo yanaweza yakaifanya siku yako ikapotea na ukaishia kufanya
mambo ambayo hayakusaidii kabisa. Inapotokea ukaiendesha siku yako bila faida
hiyo ni hasara kubwa sana kwako.
Na
mambo kuharibika katika siku yako hadi kupelekea siku yako kuharibika na kuwa
ya hovyo huwa haianzi mbali sana. Mambo yote huwa yanaanzia kwenye lile saa la
kwanza unapoamka. Saa hili la kwanza ni muhimu sana kwako.
Huo
muda au saa hilo ni wakati wa wewe kutulia na kulitumia vizuri hadi kufikia
mafanikio. Ikiwa lakini saa hilo moja utalitumia hovyo ujue kabisa utakwama na
utaharibu karibu kila kitu katika siku yako ambayo ilitakiwa iwe ya mafanikio
kwako.
Kwa
kuwa rafiki tupo pamoja na sipendi siku yako ikaishia kuwa ya kushindwa kila
siku, ipo namna ambayo unatakiwa ujue unaweza ukaifanya siku yako ikawa ya
mafanikio na hamasa kubwa. Kivipi hili linaweza likafanikiwa?
1.
Jifunze vitu vipya.
Unaweza
ukaaamua katika saa moja lako la kwanza la siku, ikawa ni wakati wako wa kujifunza
vitu vipya. Huu ni wakati ambao akili yako inakuwa ina nguvu sana na kufanya
kitu chochote na inakuwa rahisi kuweza kuelewa.
Kwa
kuanza na kujifunza vitu vipya asubuhi na mapema hiyo itakusaidia sana kukuza
au kujenga misuli yako ya kimafanikio. Wengi hawawezi kufanya hili na matokeo
yao huanza na kusoma meseji kwenye simu au ‘kuchat’ na kujibu email za watu.
Kuanza
siku yako na vitu ambavyo havikusaidii huko ni sawa na kujipoteza. Kama umeamua
kusoma asubuhi kwa ajili ya kuongeze maarifa yako, muda huu usiwe nao na
machezo hata kidogo, sema kweli kwa faida yako.
2.
Fanya mazoezi.
Asubuhi
na mapema kabla siku yako haijanza au kabla hujaanza kujihusisha na mambo
mengine, pia wakati huu unaweza ukatenga dakika chache za kufanya mazoezi ya
mwili. Unatakiwa kuelewa mazoezi ni kitu cha muhimu sana kwako.
Unapofanya
mazoezi yanaifanya akili yako iwe na hamasa ya kutenda vitu vingi. Kama una
tabia ya kufanya mazoezi, angalia siku ambayo ulifanya mazoezi ulikuwaje na pia
angalia ile au zile siku ambazo hukufanya mazoezi ulikuwaje?
Sina
shaka utagundua siku ambazo hukufanya mazoezi ulikuwa hovyo sana. Na ile siku
ambao ulifanya mazoezi akili yako ilikuwa iko sawa. hivyo unaona mazoezi ni
mojawapo ya kitu ambacho kinaweza kikaipa siku yako hamasa kubwa.
3.
Andika.
Kama
wewe ni mwandishi au hata kama sio mwandishi, ianze siku yako pia kwa kuamua
kuandika. Andika yale unayojifunza kupitia vitabu au yale unayojifunza kupitia
maisha ya wengine pia.
Kumbukumbu
ni kitu cha muhimu sana katika maisha yako leo na hata kesho. Kumbukumbu unazoweka
zinakusaidia wewe kwa leo na hata kwa baadae. Lakini si hivyo tu, zinawasaidia
na wengine kila wakiona kile unachokiandika.
Na kwa
jinsi unavyoandika inakusaidia hata wewe kujifunza na mwisho wa siku utajikuta
umeainza siku yako kwa ubora kabisa kwa sababu kutakuwa kuna kitu ambacho
umekikamilisha na pia inakusaidia kutoa ‘stress’.
4.
Pitia mambo ya msingi.
Asubuhi
na mapema ni wakati wa wewe kupitia mambo yako ya msingi. Usianze siku yako kwa
kupiga tu simu au kujibu meseji eidha iwe kwa ‘whats app’ au ‘email’,
hao utakuwa unaharibu siku yako.
Unashauriwa
kitaalamu moja ya jambo unalotakiwa kulifanya asubuhi kabisa ni kwa wewe
kupitia yale mambo ya msingi, yaani kupitia vipaumbele vyako ulivyo navyo. Kwa kufanya
hivyo kila kitu kitakuwa kinakwenda kwako kwa mpangilio.
Kwa kujifunza
mambo hayo, itakusaidia sana wewe kuweza kuifanya siku yako ikaanza kwa hamasa
na mafanikio makubwa.
Fanyia
kazi hayo na kwa makala nyingine za mafanikio kumbuka kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.