Nov 17, 2017
Sababu Tano Kwanini Watu Wengi Hawafanyi Kazi Zao Kwa Ufanisi Mkubwa.
Si
kitu cha ajabu, mara nyingi kumekuwa na malalamiko mengi kwa ‘mabosi,’
kulalamikia watu walio chini yao kwamba wanafanya kazi chini ya viwango, lakini
si hivyo tu bali wanafanya pia kwa ufanisi mdogo sana, yaani hakuna ubora.
Ni
tatizo ambalo limekuwa likiongelewa sana na kuhusishwa na uvivu, kwamba vijana
wa siku hizi ni wavivu na hawataki kufanya kazi sana na tatizo hili limekua
likikua siku hadi siku katika maeneo mengi makazini.
Je,
kwa wewe binafsi, unafikiri chanzo cha tatizo hili ni nini? Kwa nini watu
wanakwenda kazini karibu kila siku, lakini utendaji na ufanisi wao ni kidogo
sana na hata hauridhishi kwa kiasi kikubwa kuweza kuleta mabadiliko.
Kiuhalisia
zipo sababu kadhaa, ambazo moja kwa moja zinakuwa zinapelekea utendaji wa kazi
kuweza kushuka sana kazini. Sitaki kukutajia sababu nyingi sana, katika somo
hili nakutajia sababu tatu tu, kwa nini watu wengi hawafanyi kazi zao kwa
ufanisi.
1. Mwingiliano wa mambo yasiyo ya msingi.
Ufanisi
wa kazi kuna wakati unapungua sana kutokana na kuingiliana kwa mambo yasiyo ya
msingi. Kwa mfano, utakuta mtu anafana kazi moja lakini wakati huo huo akili
yake ipo kwenye kitu kingine kama simu au Tv au kuongea na watu wakati wa kazi.
Ufanisi
katika kazi na kufanya kazi katika ubora hakuwezi kuja kwa namna hii. Ndio
maana unatakiwa kila aina ya mwingiliano uweze kuutoa ili ufanisi uweze
kuonekana kwa uwazi kabisa kwenye kila unachokifanya.
Sababu
hii peke yake, ni chanzo kikubwa sana cha watu wengi kutokufanya kazi kwa ufanisi
mkubwa. Matokeo ya hili ni kuendeleza kushindwa kwenye maisha. Kama unataka
kufanya kazi kwa ufanisi na kufanikiwa, punguza mwingiliano wa mambo yasiyo ya
msingi kwako.
2. Kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Pia kuna
wakati ufanisi katika kazi unakufa kwa sababu ya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Inapofika
kipindi wewe ni mtu mmoja halafu ukawa na kazi nyingi kwa wakati mmoja ni ngumu
sana kuweza kuleta ufanisi.
Kitu
cha muhimu kuzingatia hapa, ni kufanya kazi zako kwa utaratibu. Usijipe kazi nyingi
kwa wakati mmoja, huko kutakuwa ni kujichosha na utapoteza ufanisi sana na usishangae
hutaweza kupiga hatua kwa jambo hata moja.
Siri
kubwa ya kuweza kufanikiwa na kusonga mbele, chagua jambo moja na kisha jambo hiilo
lifanye kwa uhakika sana. Nguvu na mawazo yako yote yaweke hapo mpaka jambo
lako lilete matokeo na ufanisi mkubwa sana.
3. Kukosa hamasa kutoka kwa
wanaowaongoza.
Kuna
wakati kama unafanya kazi kwenye kampuni yaani uko chini ya mtu, unaweza
ukakosa ufanisi kwa sababu ya kukosa hamasa kutoka kwa wanaokuongoza. Ni muhimu
sana kwa watu wanaokuongoza au viongiozi wakatoa hamasa kubwa.
Pengine
unajiuliza hamasa hii ni ipi? Ni muhimu na kwa viongozi pia nao kuweza kujitoa
kufanya kazi ili kuonyesha mfano. Kinyume cha hapo unaweza ukakatishwa tamaa
kwa kujiona kama hiyo kazi unayoifanya ni kazi yako tu peke yako.
Lakini
kwa kushirikiana pamoja kuanzia viongozi hadi wafanyakazi wa kawaida ingawa
kila mtu anakuwa anafanya kazi kwa sehemu yake hiyo itasaidia kukupa motisha na
mwisho wa siku kuleta ufanisi mkubwa katika kazi.
Kimsingi,
hayo ndiyo mambo makubwa matatu ambayo yanapelekea moja kwa moja watu kuweza
kufanya kazi chini ya ufanisi mkubwa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.