Nov 26, 2017
Hutakiwi Kukwepa Jambo Hili Kama Unataka Kufanikiwa Kwa Kishindo.
Vipo
vitu vingi katika safari yako ya mafanikio ambavyo hutakiwi kivikwepa hata
kidogo kama unataka kufika juu sana kwenye mafanikio. Ila kama unataka kufika
kwenye mafanikio ya kawaida tu, unaweza ukavikwepa tu hakuna hata shida.
Leo sitataka
kuzungumzia sana vitu vingi, naomba nikudokezee jambo moja tu ambalo unatakiwa kutolikwepa ila unatakiwa ujue
namna ya kukabiliana nalo ili uweze kufanikiwa kwa kishindo kikubwa.
Jambo
hili si lingine bali ni kubeba hali hatarishi au kukabiliana na hali yoyote
hatarishi ili kuweza kufanikiwa. Unaweza ukawa hujanielewa vizuri lakini
ninachomaanisha hapa ni kuchukua ‘risk’
ili uweze kufanikiwa. Mpaka hapo sina shaka tupo pamoja.
Ukumbuke
maisha yamejaa kila aina ya hali hatarishi. Huwezi kukwepa kukutana na hali
yoyote hatarishi katika maisha yako. Ukikwepa hali hii ni lazima utakutana na
hali nyingine hatarishi ambayo unatakiwa kupambana nayo mpaka kuweza kuishinda.
Kama
kila wakati unaogopa kujitoa mhanga kwa sababu ya kuogopa kujihatarisha, basi
tambua hapo ni sawa na kuchagua umeshindwa. Hutaweza kufika popote kama hauko
tayari kuchukua ‘risk’ yoyote inayokupeleka
kwenye ndoto yako.
Inatakiwa
ujitoe mhanga kweli, haijalishi unajitoa mhanga kwenye kitu gani, kwenye
malengo yako uliyojiwekea au kwenye kitu kingine chochote. Swala la kujitoa
mhanga nakukubali kupoteza baadhi ya vitu ili ufanikiwe unatakiwa kulijua kwa
ufasaha sana.
Maarifa
uliyonayo unayatakiwa kuyatumia ili kukabiliana na kila aina ya changamoto na
si kukimbia changamoto yoyote ile. Kukimbia changamoto na kuogopa kujihatarisha
hiyo inaweza ikawa ni sawa na ujinga kwako ambao utakunyima mafanikio.
Unaweza
ukajiuliza ni kitu gani ambacho utakipata hapa dunia pasipo wewe kuweza kujihatarisha.
Ukisema biashara ni lazima uweke muda na pesa zako ili upate kile unachokitaka.
Ukiangalia karibu kila kitu kwanza lazima uhatarishe ndio upate.
Kwa mfano
hata wewe, umezaliwa kwa kujihatarisha pia. Uhai ulionao vilevile wewe kama
wewe hauna uhakika nao, hiyo yote bado unaishi katika hali hatarishi. Hiyo kama
iko hivyo kwa nini usiamue ukubali kujihatarisha kwa chochote ili ufanikiwe.?
Mara
nyingi kuchukua ‘risk’ kwa kile
unachotaka kukifanya, mwisho wa siku huweza kukupa wewe unayechukua ‘risk’ hiyo zawadi kubwa ya mafanikio. Ukumbuke
tu mafanikio yote yanaanza kupatikana kwa wewe kuchukua ‘risk’ na sio kinyume chake.
Kwa hiyo
badala ya kukimbia hali hatarishi yoyote kwako, unatakiwa kujua namna ya kuweza
kukabilina nayo ili uweze kufanikiwa. Kama hautafanya hivyo utashindwa tu hata
ufanyaje, hutaweza kukwepa kushindwa.
Ukumbuke
kama nilivyokwambia mafanikio yanapatikana kwa wale watu ambao wanajitoa mhanga
sana yaani kwa watu wanaochukua ‘risk’ kama
wewe si miongoni mwao sahau kidogo kuhusu kufanikiwa, waache wachukua ‘risk’ wafanikiwe.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.