Nov 4, 2017
Jifunze Mfumo Huu Wa S2C Ili Kuikuza Biashara Yako.
Ukitaka
kufanikiwa kibiashara ni lazima uweze kubuni njia mbalimbali ambazo
zitakusaidia wewe uweze kuwa mfanyabiashara bora, huwezi kusema unataka
kufanikiwa katika biashara halafu njia ambazo unataka kuzitumia ni njia za
kihenga.
Ninaposema
njia za kihenga sijui unanielewa kweli? Maana yangu ni kwamba njia za kihenga
ni zile mbinu za ufanyaji wa biashara ambazo zimekwisha pitwa na wakati na
zimekuwa hazileti matokeo ya haraka.
Njia hizo ni
pamoja na kususubiria mteja akafuate sehemu ambayo unafanyia biashara. Njia hii
ni njia ya kihenga sana na kama bado unaitumia njia hii basi fahamu fika unajichelewesha
wewe mwenyewe.
Wafuate wateja wako kule waliko. |
Hivyo kila
wakati ni vyema ukatumia mfumo unaitwa S2C, seller to costomer. Mbinu hii ni
mfumo mpya wa kuuza bidhaa ambao unamuwezesha muuzaji kumfuta mteja mahali
alipo. Nasisitiza juu ya kuitumia mbinu hii kwa kuwa matokeo yake ni ya haraka
zaidi katika kuleta mageuzi ya kibiashara.
Nasema hivi
nikiwa na maana binadamu ameumbwa na hulka ya matumizi ya ghafla pindi aonapo
kitu kizuri machoni pake, hivyo kama utatumia njia hii ya kumfuta mteja mahali
alipo kuna uhakika kwa asilimia zote za binadamu huyo kununua kitu ambacho
hakupanga kukinunua ili mradi tu uweze kuwa na uwezo mkubwa wa kumshawishi
mteja huyo.
Hebu jaribu
kutafakari wale ambao hufanya kazi ya kunadi biashara zao katika mabasi ya
abiria, hivi wale wateja ambao huwa wananua zile bidhaa ni kwamba walipanga
kununua bidhaa hizo? Majibu ya maswali hayo utagundua ya kwamba hapana
hawakupanga kununua bidhaa hizo bali wamejikuta wakivutiwa na bidhaa au huduma
fulani ya ghafla.
Achilia mbali
wafanyabiashara wa kwenye magari hepu tuwaangalie wale vijana ambao huzunguka
mitaani kwa ajili ya kusajili la laini za simu, swali la kujiliza je,
wanachokipata ni sawa na kama wangekaa sehemu zao za kazi? usinipe jibu.
Niache bla
bla nisije poteza maana yangu ya leo, ila nilichotaka kukwambia ni kwamba jenga
utaratibu wa kumfuata mteja mahali alipo kwani kufanya hivyo ni njia bora ya
kuongeza mauzo katika biashara yako.
Faida
nyingine ambayo utaipata kwa kutumia njia hii ya kumfuta mteja ni kwamba
utakuwa na mahusiano mazuri na wateja wako, kwani wateja wako watakuwa
wanakufahamu zaidi. Hata pale ambao watahitaji huduma yako itakuwa ni rahisi
kukupata kwa sababu umekuwa na hulka ya kiwatembelea wateja hao mara kwa mara.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ndimi
afisa mipango wa mafanikio yako.
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 909 942,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.