google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 13, 2017

Unahitaji Sana Kitu Hiki Ili Kikupe Mafanikio Yako Kila Siku.

No comments :
Popote pale ulipo kuwa hapo. Chochote kile ukifanyacho kifanye kifanye kwa kumaanisha na nguvu zako zote weka hapo. Nguvu zako za uzingativu kwenye kile ukifanyacho ni muhimu sana katika kukupa mafanikio.
Kazi au kitu chochote kinachofanywa kwa kuweka nguvu za uzingativu eneo moja, kinatoa sana thamani kubwa. Umuhimu na matunda ya kazi hiyo huonekana mara moja kwa sababu unaifanya kwa umakini.
Ni hatari sana kufanya kazi au kitu chochote huku akili yako ikiwa umeigawanya katika maeneo mengi. Watu wengi wanashindwa kwenye maisha au wanafanya vitu ambavyo havina faida na matunda kwa sababu ya kutokuweka uzingativu kwa yale wayafanyayo.

Umakini wako unahitajika sana ili ufanikiwe.
Naomba kwako utambue hivi, unapoamua kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, kwa mfano, unasoma kitabu, halafu wakati huo simu yako iko wazi, unajibu meseji au unajibu simu, kwa uhakika kitabu chako hutakisoma  vizuri.
Tena wakati mwingine utakuta mtu huyo huyo anakula, lakini anataka aangalie ‘whats app’ au aangalie kitu kingine kinachofanana na hicho. Kwa mwendo kama huo ufanisi unapotea sana na hujikuta hakuna hata kitu kimoja kilichofanikiwa.
Unapokuwa na mgawanyiko wa mambo mengi, halafu akili yako iko huku au kule ni ngumu sana kuweza kutenda kile unachokitaka kwa ufasaha. Na hii ndio kasumba ambayo watu wengi sana wanayo ya kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.
Matokeo yake nini au nini kinatokea unapokuwa unataka ufanye mambo mengi kwa wakati mmoja? Kinachokutokea si kingine bali ni msongo wa mawazo, maana karibu kila kitu kitakuwa kimekwama.
Na kama ungeamaua kuweka nguvu zako za uzingativu eneo moja, basi ungeweza kukamilisha kitu, hata kama kitu hicho ni kidogo lakini ungeweza kukikamilisha na kingekupa nguvu ya kusonga mbele zaidi.
Unachotakiwa uelewe, nguvu ya uzingativu, umakini unahitajika sana kwa kile unachokifanya ili uweze kufanikiwa. Pasipo kuwa makini na kuweka nguvu hii kwa pamoja kwa kile unachokifanya ni ngumu  sana kuweza kufanikiwa kwako.
Kitu chochote ambacho ni muhimu kwako, tumia muda wako wote hapo, usiyumbishwe na kitu, kifanye kitu hicho. Kitendo cha kukimbilia kitu kingine, inaonyesha kitu hicho si cha muhimu sana kwako.
Utabadilisha sana maisha yako kwa sehemu kubwa kama kuanzia leo utaamua kuweka nguvu zako za uzingativu au kuweka umakini katika eneo moja.  Mafanikio makubwa utayaona kwenye maeneo mengi ya maisha yako kwa wewe kuwa makini.
Hivyo hatua unayotakiwa kuchukua leo, ni kuanza kuweka umakini au nguvu za uzingativu katika kila kitu, nimesema kila kitu usiache kitu chochote kipite au kifanye akili yako ikawa imegawanyika.
Anza kuweka ngvu za uzingativu kwenye kazi yako unayoifanya. Ikifika masaa ya kazi yako, jione kwa asilimia zote kwamba sasa huu ni muda wa kazi ambao nakwenda kufanya na kusiwe na mwingiliano wa aina yoyote.
Anza kuweka nguvu zako za uzingativu kwa familia yako, hapa nikiwa na maana unapokuwa na familia yako, akili yako yote weka hapo. Usifanye kosa unapokuwa na familia halafu ukajifanya wewe ndio mtu wa kuongea sana na simu, utaharibu mahusiano.
Umakini ni kitu ambacho unakihitaji sana ili uweze kufanikiwa. Utashindwa sana kwenye maisha yako ikiwa utakosa umakini au nguvu za uzingativu kwa kile unachokifanya, hivyo unatakiwa kuwa makini.
Washindi katika maisha ni watu makini na wanaweka nguvu za uzingativu katika neo moja. Tafadhari kuanzia leo kuwa miongoni mwao kwa kuweka umakini kwa kila unachokifanya na pia utafanikiwa sana.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.