Nov 10, 2017
Jinsi unavyoweza Kujua Vipaumbele Vyako Vya Kweli.
Ipo namna
rahisi ambayo inaweza kukusaidia kujua vipaumbele vyako vya kweli na hata
vipaumbele vya mtu mwingine bila hata kuambiwa. Nasema vipaumbele vya kweli kwa
sababu, unaweza ukawa na vipaumbele, lakini usipochukua hatua, hivyo sio vipaumbele vya kweli.
Najua
unaelewa kila mtu anasema ana vipaumbele
vya aina fulani na wengine vipaumbele hivyo huwa wana vitaja kwa kuvipamba
sana. Kitu cha kujiuliza je, hivyo vipaumbele vyao wanavifatilia na kuchukua
hatua?
Kama
nilivyosema ni rahisi kusema tu, ‘ooh
mimi nitafanya, hiki au kile kwa sababu ndio kipaumbele changu’. Sawa hatukatai, lakini hata useme vipi,
unaweza ukasema sana lakini mwisho wa siku vipaumbele vyako visiwe hivyo
ambavyo unaviongelea.
Ndiyo,
unashangaa, ni kweli kabisa, unaweza ukaongea sana vipaumbele vyako ni hivi, lakini
visiwe hivyo tena, kivipi hili?tutajua kutokana na utekelezaji wako,
unatekeleza kitu gani, nini ambacho unakifanya? Hapo ndipo kipaumbele chako kilipo.
Inabidi
ufike mahali uelewe, vipaumbele vyako vinaonekana si kwa kile unachokisema tu, bali
vipaumbele vinaonekana kwa jinsi namna unavyochukua hatua zako. Yale mambo
unayoyachukulia hatua na kuyafanikisha ndiyo yanaonyesha vipaumbele vyako
halisi.
Ukitaka
kujua vizuri vipaumbele vyako ni vipi, angalia vitu vinavyokuzunguka, ni kitu gani ambacho umekamilisha na kitu gani
ambacho hujakamilisha. Vile vyote ulivyovikamilisha iwe kwa mwaka huu au miaka
ya nyuma, ndivyo vipaumbele vyako ulikuwa navyo.
Kwa hiyo
ili kujua vipaumbele vya mtu huhitaji sana kusikia kile anachokisema kwa mdomo
wake, angalia vile alivyovikamilisha au subiri ni kitu gani ataanza
kukikamilisha hicho ndicho kilikuwa kipaumbele chake cha muhimu.
Unaweza
ukawa una vipaumbele vizuri sana kwa kuviongea, lakini katika utekelezaji hivyo
basi visiwe vipaumbe vyako. Vipaumbele vizuri sana kwa upande wako ni vile
ambavyo vimeshaingia kwenye mchakato au vile unavyovifanyia kazi.
Vipaumbele
unavyojiwekea au ulivyo navyo ni zaidi ya ile orodha ambayo unaiandika. Unatakiwa
ujifunze vipaumbele halisi vinapatokana kwa wewe kuweza kuchukua hatua kamili
kwenye maisha yako na sio kusema peke yake.
Kama
kuna mahali unaona huridhiki na maisha
yako na unapata matokeo ambayo sivyo, inatakiwa ubadili vipaumbele vyako
kwa kuweza kuchukua hatua zinazositahili
na si kuishia kusema tu peke yake.
Inatakiwa
ukumbuke, vipaumbele vya kweli kwenye maisha yako ambavyo vitakuletea matokeo
chanya uyatakayo vinakuja kwa wewe kuweka juhudi ,vinakuja kwa wewe kukabiliana
na kila aina ya changamoto na kujitoa hadi kuweza kufanikiwa.
Vipaumbele
hivi kwa wenzetu wazungu wanaviita ‘unspoken priorites’, yaani vipaumbele
vinavyojieleza vyenyewe, vipaumbele ambavyo huhitaji kuviongelea sana ila
matokeo yanaonekana moja kwa moja kwa nje na kwa uwazi mkubwa.
Ukweli
ni kwamba, umewahi na unaweza kuwa na viapumbele vya kweli ambavyo itakusaidia
kubadili maisha yako. Siri ya kweli ya kubadili maisha yako ni kuwa na
vipaumbele vya kweli va kubadili mfumo wa maisha yako.
Umeona
kama tulivyonaza kusema kwenye makala hii, vipaumbele vya kweli vinakuja kwa
wewe kuchukua hatua, kujitoa na hadi kuona unafanikisha ndoto zako na lakini
sio kuishia kusema sema tu kwamba hivi ni vipaumbele vyangu.
Hivyo, unachotakiwa kufanya wewe ni kupiga kazi na kuacha vipaumbele vya kweli viseme
vyevyewe. Huhitaji kuwaambia watu sana vipaumbele vyako vya kweli ni vipi au
pia huhitaji kuuliza vipaumbele vyako vya kweli ni vipi, utajua tu kwa yale
wanayoyafanya.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.