Nov 5, 2017
Jenga Mtazamo Huu, Ukusaidie Kufanikiwa Kwa Asilimia Mia Moja.
Watu
wenye mafanikio wanaishi katika dunia moja na watu ambao hawana mafanikio.
Maisha na mazingira wanayoishi watu wenye mafanikio na watu ambao hawana
mafanikio, yanafanana kwa sehemu kubwa sana.
Kwa
mfano, utakuta watu wasio na mafanikio wanaishi kwenye mazingira na changamoto
nyingi kama kukatishwa tamaa, kukataliwa sana, lakini cha ajabu hata watu wenye
mafanikio pia, wanaishi kwenye mazingira kama hayo hayo.
Unaweza
ukafikiri kiraisi sana eti tu kwa sababu wewe huna pesa au kwa sababu wewe una changamoto
nyingi, basi unajiona wewe una dunia yako na wale watu wenye mafanikio wana
kama dunia yao. Hakuna kitu kama hicho.
Tengeneza mtazamo chanya ukusaidie kufanikiwa. |
Wote
tunaishi katika dunia ile ile yenye jua lile
lile na changamoto zile zile. Pengine mpaka hapo unajiuliza sasa kama iko hivyo
ni kitu gani ambacho kinatofautisha watu wenye mafanikio na watu ambao hawana
mafanikio?
Kiuhalisia,
yapo mambo mengi yanayofanya wewe ushindwe na wengine wafanikiwe ingawa
mazingira wote mnaishi ya kufanana. Kitu kimojawapo kinachokufanya ushindwe ni
namna wewe unavyochukulia mambo.
Haijalishi
ni hali gani uliyonayo au ni kitu gani ambacho kinachokukumba, ila jinsi
unachokulia mambo nako ni muhimu sana kwa mafanikio yako. Kila jambo unatakiwa
kulichukulia kwa uchanya zaidi hata kama limekujia vibaya.
Ni
kweli sikatai changamoto katika maisha zipo na nyingi tu, lakini unapokutana na
changamoto hizo unakuwa unazichukuliaje? Je, unajiona changamoto hizo
zinakuzamisha au unaona nini?
Kama
nilivyosema ni muhimu sana kuwa na mtazamo mzuri kwa kila kitu kinachokutokea
yaani unatakiwa kuwa na ‘positive success
response’ nzuri ambayo itakusaidia kufanikiwa. Ikiwa unachukulia mambo
hovyo na wewe utakuwa hovyo tu.
Watu
wote wanaochukulia mambo kwa mtazamo chanya, watu hawa ni watu wa mafanikio kila
wakati. Uwe na uhakika utafanikiwa kwa asilimia zote kama kila kitu
unakichukulia kwa mtazamo chanya.
Hata
mambo yako yanapokwama unakuwa unaelewa, ipo siku mambo yangu yatakaa sawa,
hiyo ndiyo imani kubwa unakuwa nayo na unashangaa kweli unafanikiwa kuweza
kufikia mafanikio yako.
Kila
wakati zingatia kuwa na mtazamo chanya katika maisha yako na utafanikiwa karibu
kwa kila jambo, ikiwa mtazamo huo utauendeleza karibu siku zote kwenye maisha yako. Mtazamo chanya
ni njia sahihi ya mafanikio yako.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.