google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 15, 2017

Kila Wakati Chagua Jambo Hili, Likupe Msingi Imara Wa Mafanikio Yako.

No comments :
Badala ya kuendelea kukasirika hebu tafuta jambo la kukusaidia kukupa furaha. Kuendelea kukasirika kwako hakuwezi kukusaidia sana.
Badala ya kuendelea kuwa adui wa watu, tafuta njia ya kutafuta suluhu na kwa rafiki mkubwa wa watu, maana mahusiano bora yanalipa.
Badala ya kuendelea kuwa na wasiwasi na jambo lolote lile, jifunze kuchukua hatua ili wasi wasi huo uweze kuutoa kabisa.
Badala ya kuendelea kuwa mtu wa visasi, tafuta namna ambayo utakuwa mtu wa msamaha. Hata kama umeumizwa sana, jifunze sana kusamehe.
Badala ya kuendelea kuwawazia wengine mabaya, jenga utaratibu wa kuwaombea pia mazuri maishani mwao.



Mara nyingi nguvu hasi ni nguvu chanya ambazo zinakwenda kinyume. Kikubwa jifunze kubadilisha nguvu hasi zako kuwa nguvu chanya ili zikusaidie.
Huhitaji kuendelea kujibebesha nguvu nyingi hasi zisizo na msingi maishani mwako, unachohitaji ni kutuliza akili yako na kuanza kutumia nguvu chanya.
Hakuna mafanikio utakayoweza kuyapata kama kila wakati ndani mwako una nguvu nyingi sana hasi.
Unapokuwa una nguvu nyingi hasi, zinakuwa zinakurudisha nyuma sana pasipo wewe  mwenyewe kujua sasa unarudi nyuma.
Piga marufuku kwenye maisha yako kujibebebsha nguvu zako nyingi hasi, ili zisikupoteze wewe na wanaokuzunguka.
Kwa jinsi unavyoweza kuwa na nguvu hasi nyingi, ni vivyo hivyo utambue unaweza ukawa na nguvu nyingi chanya.
Kwa mfano, gari lenye uwezo wa kusafiri kilomita 90 kwenda mashariki, gari hilo hilo lina uwezo wa kwenda kilomita 90 nyingine magharibi.
Hata nguvu zako ulizonazo unaweza kuzinyumbulisha kwa jinsi unavyoweza wewe na kuzitumia kwa ufasaha kukupa maisha ya amani na furaha kwako na wengine pia.
Inapofika mahali unahisi una nguvu hasi kama kukasirishwa, jifunze kwanza kutulia halafu ufanye maamuzi mazuri ambayo utayatatoa ukiwa umetulia na chanya kwako.
Badilisha huzuni yako, ambayo unayo mara kwa mara, ili huzuni hiyo igeuke na kuwa furaha kubwa maishani mwako.
Badilisha kulalamika kwako na uwe mtu wa kutoa ushauri, malalamiko kwa namna yoyote ile hayafai kwako na yatakupoteza.
Badilisha uchungu ulionao ndani mwako, nao pia uwe furaha. Kujibebesha uchungu kila wakati kutaendelea kukuumiza sana.
Hali yoyote ile ambayo inaonekana mbaya kwako inaweza kubadilishwa na kuwa hali nzuri ambayo itakupa mafanikio makubwa sana.
Nguvu chanya tunazoziongelea hapa, tayari unazo ndani mwako, unachotakiwa kufanya ni kwa wewe kufanya mbinu za kubadilisha mwelekeo tu.
Haijalishi ni jambo gani limekukuta, iwe ni kupata hasara au jambo ambalo kwako unaliona ni baya, geuza ubaya huo, angalia upande wa mema au mazuri.
Kuwa na uchaguzi wa kuishi maisha chanya ni msingi mzuri sana kwako wa kukufanya uishi katika afya njema kihisia na kujenga furaha ya kudumu.
Angalia katika maisha yako, yale yote ambayo umekuwa ukiyaona mabaya, yafanye yawe mazuri na uyatumie kwa manufaa.
Kupitia wewe ambaye utakuwa sasa ni mtu wa uchaguzi wa kuamua kuishi maisha bora kwa kuwa chanya, itapelekea wengine kuiga mfumo wa maisha yako.
Kitu cha kutoka nacho hapa na ambacho unatakiwa kukifanyia kazi ni kwamba kwa hali yoyote unayokutana nayo chagua kuwa chanya wakati wote.
Kama tulivyosema hata kama kuna ubaya gani, chagua daima ‘positive altrnative’ kwenye maisha yako, hiyo itakusaidia kujenga na kusimamisha ndoto zako kwa kiasi kikubwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.