Nov 8, 2017
Rafiki Wa Karibu Wa Kukupa Mafanikio Ni Huyu Hapa.
Kama unataka kusonga mbele na kuwa na mafanikio makubwa
zaidi, mshirika wa kwanza ambaye unatakiwa kushirikiana naye bila kumwacha hadi
akakupa mafanikio hayo ni muda wako ulionao.
Ufanye muda uwe rafiki yako wa karibu sana ili
ukupatie mafanikio. Usipoteze muda wako kwa mambo ya hovyo, fanya vitu vyako
kwa umakini na mpangilio mkubwa, kila unapotumia muda wako.
Inawezekana maisha yako umekuwa ukiyaona hayafai
hasa kwa kuona hujatimiza karibu kila kitu. Hiyo inaweza ikawa ni sawa, lakini
wakati na nafasi ya kubadili mambo hayo na kuwa mazuri unayo tena.
Muda ukiutumia vizuri unaweza kukupa uwezo wa
kukamilisha mambo ambayo kwa kawaida yalionekana ni magumu kuweza kuyatimiza.
Kipi unachokitaka ambacho kitashindikana kwa sababu ya muda.
Je, unataka kuandika kitabu? andika mistari
michache kila siku, muda utafika kitabu chako kitakamilika. Je, unataka kujenga
biashara yako? anza na biashara yoyote hata kama ni ndogo sana na ikuze kidogo
kidogo, muda ukifika itakuwa kubwa sana.
Chochote unachotaka kukifanikisha kwako
inawezekana, hata iwe unataka kuongea lugha mpya? jifunze maneno machache kila
siku na wakati utafika utafanya kwa ufasaha na kujikuta mzungumzaji tayari.
Kama nilivyotangulia kusema, karibu kitu chochote unachokitaka, kipo ndani ya uwezo
wako na unayo nafasi kubwa ya kukifikia ikiwa utaamua kutenga muda wako kufanya
jambo hilo na kulifanikisha.
Rafiki wa karibu yako, rafiki
ambaye anaweza kukupa mafanikio makubwa sana
ni muda wako. Unatakiwa ukae chini na kujiuliza maswali ya msingi, je
muda wako unautumia vizuri au hovyo hovyo.
Kama unatumia muda wako hovyo,
utakuwa kwenye wakati mgumu sana wa kuweza kubadili hali ya maisha yako na hadi
kuwa nzuri. Kumbuka hata ukiwa na hali mbaya vipi, lakini ukiweka juhudi na
kujipa muda utafanikiwa.
Hakuna ambaye ameachwa mtupu,
kama matumizi ya muda wake ni sahihi. Kama ulikuwa hujaanza kutunza muda wako
kwa ajili ya mafanikio, anza leo. Fanya mambo ya kukua mafanikio hata kama ni
madogo sana, baada ya miaka michache utafanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri
wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano;
+255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.