Nov 1, 2017
Matunzo Ya Kuku Wanaotaga.
Hapa tunaangalia
majogoo na mitetea yenye umri wa kuanzia miezi minne na kuendelea.
Matunzo mengi wanayopewa
ni sawa na ya kuku wanaokua (tafadhali rejea kwenye somo la matunzo ya kuku
wanaokua).
Matunzo mengine ya
ziada:-
1. Watenge majogoo na
matetea kwa idadi inayofaa.
Kama unafuga huria,
jogoo mmoja kwa mitetea 6.
Kama unafuga kwenye
vyumba, jogoo mmoja kwa mitetea 4-5.
2. Wape chakula cha ‘layers’ chenye virutubisho vya
kutosha.
3. Endelea kuchanja
Newcastle kila baada ya wiki 10.
4. Endelea kuwapa dawa
ya minyoo kila baada ya wiki 10.
5. Walishe majani na
mboga mboga kwa wingi, ili mayai watakayotaga yawe na kiini cha njano.
6. Kuwa makini sana na
sehemu ya kifua na eneo la chini la mitetea, ambapo ndipo mayai yanapohifadhiwa
kwa ndani. Kuku akigongwa au akijigonga eneo hilo, yai linaweza kupasuka
kwa ndani, na tetea huyo atanyong'onyea, na baada ya siku kadhaa atakufa.
7. Okota mayai mara
nyingi iwezekanavyo, ili kuzuia kuku kula mayai au wasiyavunje au kuyawekea
ufa.
8. Kuku wanapoanza
kutaga nunua daftari ya kutunza kumbukumbu za mayai yanayotagwa kila siku. Hii
itakusaidia kujua siku wanapopunguza kutaga, ili kutafuta chanzo, na kama ni
ugonjwa, watibiwe haraka.
Kila la kheri katika
ufugaji wako, na endelea kuwa pamoja nasi katika masomo mengine ya ufugaji wa
kuku.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na PURE KIENYEJI. Kwa
mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767
048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.