google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 19, 2017

Kama Utang’ang’ania Sana Mpango Huu, Huwezi Kufanikiwa.

No comments :
Mafanikio mara nyingi sio rahisi kuweza kuja moja kwa moja kama vile ambavyo mipango yako uliojiwekea awali jinsi ilivyo.
Si ajabu sana utakuta unapanga kufanya kitu hiki au kile na kuwa na uhakika kabisa unafanikiwa, lakini unashangaa mambo yanaingiliana na unashindwa kutimiza lengo.
Ndio maana ili kufikia mafanikio yako unatakiwa kupanga kwa umakini sana hatua unazotakiwa kuchukua ili kufanikiwa, lakini pia unatakiwa uwe tayari kubadilika.
Ikiwa wewe mipango yako uliyoiweka au ambayo umeipanga kwamba hii ndiyo itakusaidia kuweza kukufanikisha ukaamua kuipanga kwa kuimiminia zege huwezi kufanikiwa.
Ninaposema kuimiminia zege ni kuweka mipango ambayo huwezi kuibomoa tena, kwamba ulichosema ndicho hicho na hakiwezi kubadilika.

Kama utakuwa na mipango ya kukufikisha kwenye mafanikio ya namna hiyo, mipango hii itakuchukua muda sana kuweza kuifikia.
Kila kitu kinabadilika, hata mipango ambayo unakuwa unapanga haiwezi kukufikisha kwenye ndoto zako, pia inaweza ikabadilika lakini sio swala la kuing’ang’ania sana.
Unatakiwa uelewe mipango uliyoiweka sio malengo yako, hio ni mipango tu unaweza ukaibadilisha na kufuata mpango mwingine bora.
Ni sawa na wewe uwe unataka kwenda mjini na gari lako halafu gari likaharibika, je jiulize hutaweza kwenda mjini mpaka gari lako lipone, sina shaka hapana.
Najua tu hapa utaamua kutumia njia nyingie ikiwa pamoja na hata kuita teksi ili ikufikishe kule unakotaka kufika na kwa ule muda ulioupanga na sio kuendelea kubakia hapo.
Ikiwa wewe utaendelea kung’ang’ania mpango wako wa awali ukusaidie kufanikisha tu hata kama ni mbovu basi utakuwa ni mtu ambaye umeamua kuchagua njia ndefu sana ya kufanikiwa kwako.
Unachotakiwa kujua ni kwamba mpango wako mmoja unapokataa, uwe na mpango mwingine mbadala wa kuweza kukusaidia wewe kufikia ndoto zako.
Kuwa na mpango mmoja tu ambao unasema unaamini na kuamua kuziba masikio na kuacha kila kitu hii ni hatari kubwa sana kwako.
Badilika kulingana na mazingira, na pia unatakiwa kubadilika kulingana na wakati wa utekelezaji wa ndoto zako.
Ikiwa hautafanya hivyo andika utashindwa tu. Usikubai kutumia njia ndefu kufikia mafanikil yako kwa kung’ang’ania pengine mpango mbovu kwako, UTAKWAMA.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote manakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.