google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 3, 2017

Ili Kuzishinda Changamoto Za Kimaisha, Kijue Kwanza Kitu Hiki…?

No comments :
Vitu vinabadilika. Watu wanabadilika. Sheria zinabadilika. Mazingira yanabadilika pia. Mabadiliko yapo kila wakati na kila mahali. Kile ulichokiona jana, leo hakipo hivyo na kesho pia hakitakuwa hivyo kwa sababu ya mabadiliko.
Fikiria wale watu unaowajua. Je, unafikiri ni watu wale wale kama ulivyokuwa ukiwajua mwanzo na wanaendelea na maisha na mienendo ileile? Sina wasiwasi, lazima yapo mabadiliko kwa watu hao.
Jaribu kufikiria tena, mambo ambayo umeyabadilisha wewe mwaka mmoja nyuma, kama unaona yapo mabadiliko ya aina fulani, basi yote hiyo inaonesha kwamba mambo yanabadilika kwenye maisha kila kukicha.
Kumbuka mabadiliko yapo, hata wewe unabadilika pia. Ikiwa utakuwa ni mtu wa kukataa mabadiliko, basi changamoto za maisha zitakusumbua sana. Unatakiwa uendane na mabadiliko ili kuzishinda changamoto za kimaisha.

Watu ambao hawabadiliki, watu ambao hawataki kuendana na mabadiliko, sio rahisi sana kupiga hatua. Maisha yao yako vile vile miaka nenda rudi, tena zaidi yanakuwa magumu sana.
Nakumbuka kuna watu ambao nawafahamu tokea nipo kidato cha kwanza, zaidi ya miaka 15 nyuma, watu hao maisha yao yako vile vile, nikiwa na maana shughuli wanazofanya ni zile zile, ambazo haziwafikishi mbali.
Kitu gani kimetokea kwa watu hawa hadi kuwa na maisha yale yale ambayo hayabadiliki kwa zaidi ya miaka 15, si kingine bali kugomea mabadiliko. Ni kitu hatari sana kama hujui umuhimu wa mabadiliko maishani mwako.
Hebu jiulize mimea inabadilika, dunia inabadilika kila siku, kipi kinachokufanya usishutuke na kuamua kubadilika? Kuendelea kubakia vile vile na kutokufanya mabadiliko yoyote kwenye maisha yako ni kujiweka kwenye hatari kubwa sana.
Kila siku unatakiwa uwe mpya, kila siku unatakiwa kubadilka kwa kujifunza vitu vipya. Usipobadilika uwe tayari kuachwa nyuma tena mbali sana na hali ambayo itasababisha maisha yako yarudi nyuma sana.
Hakuna mtu ambaye ni mpinga mabadiliko halafu akafanikiwa. Watu wote ambao hawataki kufungua akili zao na kuamua kubadilika ni watu wa kukwama sana maishani mwao karibu kwenye kila kitu wakifanyacho.
Hutakiwi kuionea huruma akili yako linapokuja swala la mabadiliko katika maisha  yako. Kwa kawaida akili yako haitaki shida sana, akili inapenda ipate vitu vya kuburudisha na ndio maana mabadiliko yanakuwa magumu kwako kutokea.
Huhitaji kumtafuta ‘mchawi’ wa mtu aliyefanya maisha yako kuwa mbaya leo, ‘mchawi’ wa kwanza ni wewe. Anza kufanyia kazi mabadiliko yanayojitokeza maishani mwako ili ujenge maisha ya mafanikio makubwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.