google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 5, 2017

Usikwamishwe Na Chochote Kwenye Maisha Yako...Endelea Kuchukua Hatua.

No comments :
Ni kitu gani utakifanya leo kwa uhakika sana, ikiwa utajua kwamba kila utakachokifanya kinakwenda kufanikiwa moja kwa moja? Ni kitu gani utafanya?
Najua leo ukiambiwa kuna kitu ukikifanya kitakua na mafanikio ya moja kwa moja, basi lazima kuna kitu ambacho utakichagua kukifanya kwa moyo wote.
Hebu jiulize tena ni kitu gani utakwenda kukifanya, ni mradi gani utakaoamua kuufanya au ni biashara gani utakayoifanya ikiwa utahakikishiwa mafanikio kwa asilimia zote?
Je, kuna kitu unaogopa kukifanya kwa sababu ya kuogopa kushindwa? Je, kuna kitu chochote unakiogopa kukifanya kwa sababu ya maneno ya watu?
Nikwambie hakuna uhakika wa asilimia zote wa kupata mafanikio moja kwa moja, mafanikio utayapata kwa kujaribu mara nyingi uwezavyo.

Bila kujali matokeo, fanya kazi yako kwa moyo wote.
Uhakika ambao naweza nikakupa ni kwamba, utashindwa na utaendelea kushindwa sana ikiwa wewe utakuwa unaogopa kuchukua hatua kwenye maisha yako.
Kuchukua hatua na kufanya bila kujali utashindwa au kufanikiwa ni njia nzuri sana ya kukufanikisha. Hata ukishindwa sio mbaya utakuwa pia umekua kwa kujifunza.
Unatakiwa kuamini uwezo mkubwa ulio ndani yako nakuendelea kufanya, kuliko kusubiri mtu mwingine akwambie unaweza eti ndio ufanye.
Ili kufanikiwa unatakiwa kuendelea kufanya, ili kufanikiwa unatakiwa kuendelea kuchukua hatua bila kujali matokeo ya sasa unayoyapata ni matokeo ya aina gani.
Unapochukua hatua kwa kufanya unakuwa unajifunza vitu vingi sana ambavyo vinakusaidia kufanikiwa zaidi kuliko ambapo ungetulia.
Unatakiwa kuanza sasa kuendelea kufanya kile unachikiamini kwamba kitakusaidia kwenye mafanikio yako kuliko kuogopea mbali.
Kuogopa unakogopa hakuwezi kukusaidia kitu zaidi kutakuangushha, ukizingatia hakuna mtu ambaye amewahi kufanikiwa kwa kuogopa.
Watu wote wanaofanikiwa, wanafanikiwa kwa sababu ya kuchukua hatua tu na sio vinginevyo hata kidogo.
Kwa hiyo unachotakiwa kuelewa hapa ni kuendelea kujituma kwa kufanya, siku hadi siku  na hapo utajiweka kwenye wakati mzuri na bora wa kujenga mafanikio yako.
Hakuna kitakachoshindikana ikiwa utaamua kuendelea kuchukua hatua kwa kufanya. Usiamini sana kwamba kwa chochote unachokifanya kitashindwa.
Ushindi wa mafanikio upo mbele yako ikiwa unachukua hatua na kufanya. Usikubali kukwamisha na kizuizi au kitu chochote, endelea kufanya matokeo bora utayaona.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.