google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 20, 2017

Usifanye Kosa La Kuwekeza Nguvu Hizi Tu Basi Kwenye Mafanikio Yako.

No comments :
Ili kufanikiwa kwa chochote kile unalazima kwa wewe kuanza kwanza jambo hilo. Hakuna kitu au mafanikio ambayo utayapata kama utabaki tu kuongelea mafanikio mdomoni. Kuanza ni lazima uanze bila kujali unaanza kwa namna gani.
Lakini hata hivyo kuanza peke yake hiyo haitoshi na wala hiyo siyo 'gerentii' ya mafanikio, unahitajika kuendelea kuongeza juhudi zaidi za kuweza kufanikiwa kwa kufanya kazi kila siku. Juhudi endelevu ni muhimu kwa mafanikio yako.
Watu wengi wanaanguka sana kwenye vile vitu wanavyofanya kwa sababu wanakuwa ni watu ambao wakati wanataka kuanza walikuwa ni watu wa juhudi sana, lakini mara tu wanapoanza, hujikuta wanajisahau na juhudii zile kuziacha mara moja.

Sasa inapotokea ukafanya hivi yaani ukaweka juhudi kubwa mwanzoni na mbeleni ukajisahau, kupiga kwako hatua inakuwa ni ngumu. Mafanikio yako ni rahisi yakaonekana kwenye hatua za mwanzoni huko mbele hakitaonekana kitu tena kama hutaendeleza juhudi.
Kwa hiyo kama unataka kufanikiwa unatakiwa kukumbuka kila mara kuweka juhudi mwanzoni lakini na kuendelea kuweka juhudi hizo hizo kwenye kila hatua unayopitia. Hiki ni kitu muhimu sana na msingi sana kwa mafanikio yako.
Ndio maana siku zote huwa tunasisistiza unapotaka kuanzisha jambo acha kujiandaa sana, unapokuwa unajiandaa sana hiyo itakupelekea wewe kutumia nguvu nyingi mwanzoni na kujisahau kufanya majukumu ya msingi mbeleni.
Watu wengi wamejikuta katika mtego huu wa kushindwa kufanikiwa sana kwenye kila wanachokifanya kwa sasa kwa sababu tu ya kujivunia nguvu kubwa walizoweka mwanzoni na kusahau kuweka juhudi hizo mbeleni tena.
Ili kuelewa hili vizuri, angalia mfano mzuri wa miti mikubwa. Miti hii huwa inaanza kama kitu kidogo tu. Lakini katika kuendelea kukua hurefuka na mwisho wa siku kuwa mti mkubwa sana ambao kuukata inahitajika nguvu nyingi sana.
Halikadhalika, hata mto huwa unaanza kidogo kidogo lakini kwa jinsi unavyozidi kwenda mbele unakuwa una nguvu kubwa ya kuweza kusomba chochote kile kinachoweza kukatisha mbele.
Vivyo hivyo na wewe ndio unatakiwa kuwa hivyo. Anza na nguvu fulani hata kama sio kubwa sana, lakini nguvu hiyo endelea kuiwekeza ili iwe kubwa zaidi na zaidi. Kama hautafanya hivyo mafanikio yako yatakuwa ya muda tu na kutoweka mara moja.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.