google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 15, 2017

Makosa Wayafanyayo Wafugaji Kabla Ya Kuingiza Vifaranga.

No comments :
Yapo makosa ya wazi ambayo baadhi ya wafugaji huyafanya wakati wanapoagiza vifaranga. Haya ni makosa ambayo hutakiwi kuyafanya mara kwa mara ukiwa mfugaji kwani ukifanya yatasababisha kuku wako wengi kufa.
Ni matumaini yangu kuwa kusoma makala haya utajifunza makosa haya na kuyaepuka kabisa na kufanya ufugaji wenye tija kwako.

1. Kutokuwa na ratiba ya kufanya usafi na maandalizi mengine ya banda mapema
2. Kununua vifaranga kabla hujamaliza kujenga banda.
3. Kutokuwakagua vifaranga kule unapowachukua kama wana kinyesi kilichoganda.
4. Kutokutunza chakula vizuri, na kuacha chakula kikaliwa na panya, ambao wanaweza kukichafua na kuwasababishia magonjwa vifaranga.
5. Kujenga banda dogo sana ambalo ni vigumu kulifanyia usafi.
6. Kununua vifaranga vingi kuliko eneo la banda lako.
7. Kuchukua aina ya kuku ambayo haiendani na hali ya hewa ya eneo ulilopo.
8. Kutokuandaa dawa za mwanzo za vifaranga.
9. Kutotumia dawa ya kuua wadudu na bakteria wakati wa kusafisha banda.
10. Kutokupata elimu ya kutosha juu ya ufugaji vifaranga vya kuku.
11. Kuandaa banda la vifaranga lililofungwa sehemu zote, yaani hewa haizunguki.
12. Kutoziba mashimo na matundu, kuacha mlango wa banda wazi, hivyo panya, paka, mbwa na vicheche wanaweza kuingia.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote manakaribishwa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.