google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 28, 2017

Huu Ndiyo Ujasiri Unaotakiwa Kuwa Nao Ili Kuzishinda Changamoto Zako Mara Moja.

No comments :
Haijalishi maisha yako uliyonayo yakoje, yaani ya mafanikio sana au ya kushindwa sana, lakini jambo ambalo ni lazima utakutana nalo kila wakati ni changamoto.
Changamoto katika maisha zipo kwa kila mtu, haziangalia hali ya kipato au kitu chochote, changamoto zipo na zinatofautiana.
Ujasiri unaotakiwa kuwa nao ni kuzishinda changamoto hizo na kuamua kuweza kusonga mbele bila kujali ukubwa wa changamoto hizo.
Lakini ikiwa kila wakati utaamua kutulia na kuchelewa kutatua changamoto zako mapema, ujue unaongeza changamoto zingine tena.

Kivipi, sikiliza, kila ukiona unachangamoto ya aina fulani, ujue kabisa nyuma yake ipo changamoto nyingine ambayo unatakiwa uivuke na kuifanikisha.
Ukiona unakutana na changamoto halafu unajipa muda kwamba utaitatua baadae, ujue basi kabisa unakaribisha changamoto zingine nyuma yako.
Kila unapokutana na changamoto, unatakiwa ujue nyuma yake ipo changamoto nyingine, hivyo unatakiwa kuitatua changamoto uliyonayo haraka maana nyingine zitakuja tu iwe unataka au hutaki.
Uwezo wako wa kutatua changamoto haraka ndiyo utakao kufanya uzidi kuwa mshindi. Hakuna anayeomba kukutana na chagamoto, lakini changamoto zipo na zinataka majibu.
Zipo changamoto katika fursa tunazokutana nazo na pia zipo changamoto tofauti tofauti tunazokutana nazo kwenye maisha, hizi zote tunatakiwa kuzitatua.
Ikiwa unakutana na changamoto, kisha unasema utakuja kuzitatua kwa wakati fulani, wewe elewa kabisa utakuwa unakaribisha changamoto zingine zaidi.
Kitu ninachotaka uelewe hapa ni kwamba kila unapokutana na changamoto, itatue haraka changamoto hiyo kabla changomoto nyingine haijakufikia.
Ujasiri unaotakiwa kuwa nao katika changamoto ni kuamua kuzikabili changamoto zako na si kuzipa nafasi ya baadae kwamba utazitatua kesho au siku nyingine.
Kujipa muda kwamba changamoto zako utazitatua wakati mwingine huko ni sawa kuamua sasa kwamba changamoto zako zikumalize.
Na kwa bahati mbaya sana unaweza ukaona ni kitu cha kawaida tu kwako kuahirisha changamoto, lakini changamoto hizo zikizidi ndio utajua umuhimu wa kutatua changamoto haraka sana.
Ukumbuke hata mafanikio yanakuja si kwa sababu hakuna changamoto, bali mafanikio yanapatikana kwa kutatua changamoto zako mapema sana.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.