google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 4, 2017

Chukua Hatua Mapema…Utoe Matatizo Haya Maishani Mwako.

No comments :
Tatizo kama tatizo lenyewe kwa jinsi lilivyo, haliwezi kuondoka tu hivi hivi kwa kukaa tu, bali tatizo unaweza ukaliondoa kwenye maisha yako kwa kulifanyia kazi.
Kwa mfano unaweza ukawa una tatizo la kuwa na kipato kidogo au kwa ujumla huridhiki kabisa na maisha yako yalivyo.
Unapokuwa na tatizo kama hili au hata na mengine yanayofanana hivi, elewa tu hayawezi tu kuondoka hivi hivi yenyewe, lazima utafute fursa ya kukutoa.
Tunapozungumzia tatizo kwa mfano la kiuchumi, ni fursa pekee ya kibiashara au kilimo ndio inaweza kutatua na wewe ukabaki salama kiuchumi.
Ikiwa utakuwa umekaa na kushindwa kuchangamkia fursa ambazo zinaweza zikakusaidia kuondoa tatizo lako basi, haliwezi kuondoka lenyewe.

Chukua hatua za mafanikio yako mapema.
Na kwa jinsi unavyoendelea kukaa chini na kusubiri eti upo muujiza au yupo mtu atakuja kukutoa kwenye tatizo lako, ndio tatizo hilo linazidi kuwa kubwa.
Kama nilivyosema huhitaji kusubiri, unahitaji kulitatua tatizo lako mara moja, unaposubiri unakuwa unajipotezea muda mwenyewe na kujiongezea matatizo zaidi.
Hata inapotokea fursa ambayo unaona kabisa inakusaidia kutatua tatizo lako, usichelewe sana kuitumia, kwani itakukimbia na kwenda kwa mtu mwingine.
Fursa kwa jinsi ilivyo, ina uwezo wa kutoka kwako na kwenda kwa mwingie ikiwa hautaifanyia kazi mapema na ikiwa wewe ni mtu wa kujishaua.
Acha kulaza akili yako tena, ni wakati ambao unatakiwa sasa usimame imara kutatua kila tatizo linakuzunguka.
Jukumu hutakiwi kumwachia mtu mwingine bali ni wewe. Ila kama unasubiri eti changamoto zako au matatizo yako yaje yaondoshwe na mtu unajidanganya.
Ukiweza kutatua changamoto zako mapema sana, basi akili yako inakuwa na uwezo wa kutatua changamoto nzito zaidi kadri siku zinavyokwenda.
Muda ni kitu cha thamani kwako sana, hivyo usipoteze muda wako kukaa tu bila kushughulika na changamoto inayokuzunguka.
Unatakiwa kila siku, tenga muda wa kutatua tatizo lako hata kama ni kwa kidogo sana na utashangaa unasogea na mwisho wa siku utatoka na kufanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.