google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 1, 2017

Changamoto Ulizonazo Sio Sababu Kubwa Ya Wewe Kushindwa.

No comments :
Moja ya tatizo kubwa walilonalo watu wengi hasa linapokuja swala la kutafuta mafanikio, ni kule kuchukulia changamoto ni kizuizi kikubwa sana cha kuweza kufanikiwa kwao. Utakuta mtu anaposhindwa jambo atakupa sababu au changamoto nyingi sana zilizomfanya ashindwe.
Ni kweli sikatai changamoto hizo zinaweza zikawa ni nzuri na za kweli kabisa kwao, lakini je, hiyo hasa ndio sababu ya kushindwa kwao kwa watu hao? Au je, kila anayefanikiwa ni mtu ambaye hana changamoto kabisa na wanaoshindwa ndio wana mzigo mkubwa wa changamoto maishani mwao?
Ukifanya uchunguzi utagundua kitu hiki, hizo changamoto ambazo zimekuwa zikitajwa sana kama ndio sababu zimekuwa zikitumiwa kama kisingizio tu cha kushindwa kufanikiwa kwao. Lakini ukweli sababu kubwa ya kushindwa kufanikiwa zipo ndani mwao wenyewe na si kinyume cha hapo.

Pengine wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya tabia zao mbovu au kukosa kuwajibika au hata wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi ya mafanikio. Hivi ni vitu vidogo vinavyoweza kumfanya mtu akashindwa lakini kwa sababu ya kutokujua akasingizia changamoto tu.
Ukiangalia miongoni mwa watu wenye mafanikio, wanafanikiwa sana si kwa sababu hawana changamoto au vizuizi vinavyowazuia kufanikiwa, bali wanafanikiwa kwa sababu wanaweza kupambana na changamoto hizo na kuzishinda. Kuendelea kung’ang’ania kukabiliana na changamoto ndiko kunakowasaidia.
Kila siku watu hawa wamekuwa ni watu wakuchukua hatua kwenye zile changamoto zao, bila kujali changamoto hizo ni ndogo au kubwa na kwa kufanya hivyo imekuwa ikiwasaidia sana kuweza kuwa washindi kimafanikio. Watu hao waliofanikiwa si watu wa kulialia ni wanapambana na changamoto zao kweli.
Unaweza ukajiuliza mwenyewe changamoto zako ni zipi zinazokuzuia ushindwe kufanikiwa? Je, unaziona changamoto hizo ndio kama kizuizi kikubwa kabisa cha kukufanya ushindwe kufanikiwa? Au unapokutana na changamoto ni kitu gani hasa ambacho unakuwa unakiwaza sana?
Labda nikukumbushe tu hivi, kila mtu aliyepo duniani anakutana na changamoto kwa wakati wake, lakini wanapigana na kuzishinda. Kama changamoto zingekuwa ndio sababu kubwa ya kushindwa, basi hakuna mtu ambaye angekua kafanikiwa duniani, kila mtu angekuwa kashindwa.
Sasa jiulize ushindi unakujaje katikati ya changamoto? Ushindi unakuja kwa kuendelea kupambana na changamoto lakini pamoja na kuongeza juhudi zaidi na zaidi. Na huo ndio ukweli, bila changamoto huwezi kukua sana, lazima changamoto ziwepo ili zikukomaze na kukupa nguvu ya kusonga mbele kwa kishindo kikubwa.
Kwa hiyo unapokutana na changamoto yoyote usihuzunikie au kulia. Tafuta njia ya kuondokana na changamoto hiyo hadi kufanikiwa. Kama  usipotafuta njia hiyo huwezi kufanikiwa. Kila kitu unachokifanikisha ukumbuke kina changamoto zako. Kama hilo lipo pigana na changamoto zako uwe mshindi na usizifanye zikawa sababu ya kushindwa kwako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.