google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 7, 2017

Chochote Unachokitaka Utakipata, Ikiwa Utazingatia matumizi ya nguvu hizi kubwa ulizonazo ndani mwako.

No comments :
Sijui sana kama unajua una nguvu kubwa sana za kuweza kukusaidia kufanikisha jambo lolote unalo lihitaji katika maisha yako. Nguvu hizo unazo, bila kujali unajua kivipi au hujui lakini nguvu hizo zipo ndani mwako.
Ushahidi wa kutosha upo, unaonyesha nguvu hizo zipo, ndio maana, chochote unachokitaka ukiamua na ukapanga kweli, unaweza kukipata au maisha yako yapo hivyo yalivyo kutokana uwezo ama matumizi ya nguvu zako.
Mpaka hapa naona unashangaa na unajiuliza sasa nguvu zangu nitazijuaje au zipo kwenye nini? Sikiliza nguvu zako kubwa ulizonazo, zipo kwenye mambo makubwa matatu ambayoyapo ndani ya uwezo wako mwenyewe.
1. Mawazo uliyonayo.
Nguvu zako nyingi ulizonazo na ambazo zinaweza kufanya kitu chochote ukitakacho, zinaanza kwenye mawazo yako kwanza. Mawazo yako  yana nguvu na kuumba kitu chochote unachokitaka na kikaonekana kwa nje.
Hebu jiulize ni kitu gani ambacho hakija anzia kwenye mawazo? Kila kitu unachokiona kipo duniani kwanza ni matokeo ya mawazo. Unapoona gari au majumba  makubwa hayo ni mawazo ya watu. Ukizingatia matumizi ya mawazo vizuri, utafanikiwa sana.

Maamuzi sahihi ni muhimu kwa mafanikio yako.
2. Maamuzi uliyonayo.
Nguvu nyingine kubwa uliyonayo ndani mwako ambayo ukiitumia vizuri itakupa chochote ukitakacho ni maamuzi uliyonayo. Maamuzi yako ni ya muhimu sana katika kufikia mafanikio yako unayoyataka.
Angalia ni kitu gani unachokipata bila kuwa na maamuzi, utaona karibu kila kitu baada ya kuwa kwenye mawazo yako ni lazima kwanza ukifanyie maamuzi ambayo yatakupelekea ufanye kitu kile. Hakuna mafanikio utakayapata bila kuamua.
3. Hatua ulizonazo.
Umeona mawazo ulionayo na maamuzi uliyonayo ni mojawapo ya nguvu kubwa uzilizona ndani mwako za kimafanikio. Lakini hata hivyo nguvu hizo haziwezi kufanikiwa bila kuchukua hatua. Inabidi ifike mahali uamue kuchukua hatua ili kufanikiwa.
Hatua unazozichukua ndizo zitakazokufanya uweze kufanikiwa. Hata uwe na mawazo mazuri na maamuzi mazuri vipi lakini itakulazimu uweze kuchukua hatua ili hatua hizo zikuletee uhalisia wa kile unachokitaka kwenye maisha yako.
Kumbuka, mawazo uliyonayo, uamuzi unaouchukua na hatua unazozichukua ni moja kati ya nguvu kubwa sana za kimafanikio ambazo unatakiwa uzitumie ili uweze kufanikiwa. Kwa kumiliki kwako nguvu hizo utakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kufanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.