google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 17, 2017

Tawala Matokeo Ya Mafanikio Yako Kwa Kufanya Jambo Hili.

No comments :
Upo uhusiano mkubwa sana kati ya hatua unazochukua na matokeo unayoyapata kwenye maisha yako. Ni jambo la kujiuliza wewe mwenyewe je, unalipa gharama au unavuna matunda kutokana na hatua unazochukua.
Yapo mambo mawili ambayo yanaweza kukutokea kutokana na hatua unazozichukua kama nilivyokuelezea. Mambo hayo yanaweza yakawa eidha ni kulipa gharama kutokana na hatua ulizochukua tayari au kufaidi matunda, yote inawezekana.
Kila hatua unayoichukua kwenya maisha yako ni ya muhimu sana. Ndiyo maana kila wakati unatakiwa kuhakikisha unachukua hatua zinazostahili katika kubadilisha maisha yako pasipo kujali hatua hizo ni ndogo au kubwa.

Kwa hiyo unaona upo uhusiano wa wazi kabisa kati ya hatua zako na matokeo unayoyapata, hivi ni vitu viwili ambavyo huwezi kuvitenga. Ni lazima upitie hatua za aina fulani ndio upate matokeo ya aina fulani.
Mara nyingi, wengi wetu tunapoteza muda sana kwa kufanya vitu ambavo havitupi matokeo yale tunayoyataka. Hebu angalia kwa mfano wale wanaotaka utajiri wa haraka kwa kuamua kucheza bahati nasibu, hizo kweli ni hatua lakini hazina msaada wa moja kwa moja.
Matokeo ya kucheza bahati nasibu hata ukipata hata hivyo pesa hizo hazidumu sana kutokana na kujengwa katika msingi mbovu ambao haukuweza kuhusisha hatua zinazotakiwa kuchukuliwa ili kupata matokeo.
Hakuna uchawi au kingine kinachotokea hasa pale unapoona wale watu waliocheza bahati  nasibu pesa zao kama zikipotea. Uchawi mkubwa au balaa huwa linaanzia huku kutokana na kushindwa kuchukua hatua.
Ni jambo ambalo haliingii akilini kwa kutaka matokeo makubwa sana lakini hakuna hatua kubwa ulizochukua. Kwa hiyo unatakiwa uelewe ni kwamba matokeo na hatua unazochukua ni vitu viwili ambavyo vinakaa pamoja.
Kwa lugha nyingine naweza nikasema matokeo na kuchukua hatua ni kama vile sarafu, lazima pande zote mbili ziwepo ili sarafu iweze kukamilika kwa uhakika. Acha kujidanganya kusubiri matokeo wakati huna ulichokifanya.
Kuanzia leo chukua hatua sahihi na hapo pia utapata matokeo sahihi kwenye maisha yako. Huhitaji sana kujilaumu kama mambo yako yamekwenda hovyo, chukua hatua sahihi na upate matokeo sahihi. Tawala matokeo ya mafanikio yako kwa kuchukua hatua.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.