google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 8, 2017

Majibu Ya Mafanikio Ni Muunganiko wa Mambo Haya.

No comments :
Mara nyingi hulka yangu ipo katika misingi ya kuwashirikisha watu mambo ya msingi yatakayowafanya watu hao waweze kupiga hatua za kimaisha. Hivyo naomba kama ilivyo ada yangu, naomba  nikushirikishe elimu hii ya maisha ambayo itakusaidia kuweza kupiga hatua, hivyo naomba uwe nami mwanzo hadi mwisho wa makala haya.
Na siku ya leo nataka kusema nawe kuuhusu ukweli ambao unatakiwa kujua ili kutimiza jambo fulani katika maisha yako. Na ukweli huo ni huu hapa.
Kama ujuavyo katika safari yako ya mafanikio ni lazima kuwe na vitu vikuu vitatu ili uweze kutimiza jambo lako muhimu. Vitu hivyo vitatu ni, kwanza unatakiwa kuwa WAZO, pili unahitaji UWAJIBIKAJI juu ya jambo hilo, jambo la tatu mara baada ya hivyo vyote kufanyika kinachotea huitwa MATOKEO.
Mara nyingi watu wengi huwa tunaangalia katika matokeo pekee yake huku tukisahau ya kwamba matokeo ya jambo fulani kutokea ni mnyumbuliko ambao huanza na wazo, uwajibikaji kisha kuja hayo matokeo. Ukisoma vizuri kitu ambacho kinaitwa ‘power of cause anda effect’ utaelewa vizuri.

Kwa kifupi ni kwamba ukweli juu ya nguvu ya chanzo na madhara ipo katika kuangalia madhara kuliko kuangali chanzo cha madhara hayo kutokea. Kwa mfano, ukifeli katika jambo fulani, watu wengi huwa wanaangalia pale walipoangukia pasipo kuangalia chanzo cha wao kufeli.
Hivyo ili uweze kuwa bora katika maisha yako jijengee utaratibu wa kuanza kutazama chanzo cha jambo fulani kutokea kisha uje utazame matokeo ya jambo hilo. Kitendo cha kuanza kutazama chanzo cha jambo fulani kutokea humsaidia mtu kuweza kuwa bora zaidi na pia humsaidia mtu kujua nini chanzo cha kufeli kwa jambo fulani.
Na kama ambavyo nilivyosema hapo awali ya kwamba katika safari yako ya mafanikio kuna vitu vitatu ambavyo ni lazima kila mmoja wetu  aweze kuvifahamu, vitu hivyo nimeshaviorodhesha hapo awali, hivyo kitu cha kwanza sitakuzungumzia siku ya leo,  bali nitazungumzia jambo la pili na tatu.
Mara nyingi mara baada ya kupata wazo fulani ili uweze kuanza kulifanyia kazi wazo hilo, jambo ambalo linafuata ni kuweza kuwajibika juu jambo hilo. Na katika kipengele hiki cha kuwajibika unahitaji kuwekeza nguvu na juhudi za kutosha katika kufanya kazi ili kupata majibu unayostahili.
Ukishindwa kuwajibika vizuri, basi tambua fika jambo la tatu haliwezi kuleta  matokeo ya majibu ambayo uliyatarajia. Mara nyingi upatikanaji wa majibu kwa kwa kile ambacho unakifanya hutokana na wazo na uwajibikaji wako.
Unaweza ukawa na wazo zuri ila kama uwajibikaji wako ni mdogo basi fahamu fika ya kwamba matokeo ya jambo hilo utakuwa ni finyu pia. Swali la msingi linaweza kuja, sasa nifanyaje ili niweze kufanikiwa?
Swali hilo majibu yake ni haya, kwanza hakikisha unakuwa na wazo bora ambalo limechambuliwa vizuri, lakini pia muhusika wa wazo hilo ni lazima aweze kujitoa kikamilifu katika kuwajibika ili kuhakikisha linaleta matokeo mazuri.
Mwisho nimalize kwa kusema MAWAZO MAZURI + UWAJIBIKAJI = MATOKEO MAZURI.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757 909 942,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.