google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 13, 2017

Kama Utafanya Mambo Haya, Ndiyo Yatakayokupa Mafanikio Yako.

No comments :
Hivi umeshawahi kutaka kufanya jambo la aina fulani, halafu akili yako ikagoma na kuona kabisa jambo hilo haliwezekani? au umeshawahi kuona watu wakisema kwamba aah jambo lile sio rahisi sana kuweza kulifanikisha?
Najua kitu cha namna hiyo umewahi kukiona. Lakini leo nataka uende kinyume, kwa kujifunza kufanya yale mambo ambayo yanasemwa sana kwamba hayawezekani au hayafanyiki. Naelewa umesikia sana ikisemwa jambo hili ni gumu au haliwezekani kufanyika.
Unaposikia kwamba jambo hili gumu au kufanyika kwake ni kazi kubwa sana, basi hapo ndipo kuna mavuno ya mafanikio, hapo ndipo kuna njia ya wazi ya kuweza kukusaidia kufanikiwa ipo, kuliko kukimbilia ile sehemu rahisi unayoiona.
Hebu jaribu kufikiri ambapo kila mtu anasema hawezi kufanya jambo fulani, halafu wewe ndio mtu pekee unasema naweza, kitu gani kinatatokea hapa? Ni lazima utafanikiwa na hakuna kitakachokuzuia.

Mara nyingi mafanikio yoyote yale yanakuja kutokana na kufanya mambo ambayo watu wengi hawewezi kufanya. Kama jambo unalolifanya kila mtu analifanya, kufanikiwa kwake inakuwa ni ngumu kwa sababu ya ushindani wake unakuwa mkubwa.
Kuwa mtu ambaye unathubutu, kuwa mtu ambaye utajitoa muhanga kufanikisha jambo lile ambalo kila mtu anasema hawezi. Huhitaji maarifa ya ziada au kitu kingine tofauti, ni wewe tu kuamua kujitoa na kusema moyoni mwako kwamba naweza.
Kitu kinachokufanya ushindwe kufanya mambo ambayo unaona kama hayawezekani kinakuja kutokana na wewe kujidharau na kujiweka pembeni na kuamini kwamba kuna watu fulani ambao ni kama wateule ndio eti wanaweza.
Ninachotaka kukwambia ni hivi, hata wewe unaweza. Amua kuchukua hatua na kukubali kufanya kila linawezekana kufanya yale mambo ambayo yamesemwa hayewezekani. Tenga muda wako, na hakikisha unafanyia kazi jambo hilo na litafanikiwa kweli.
Kuendelea kulaumu na kulalalamika kila siku, kutaendelea kukuweka kwenye hali mbaya. Kubali kukutana na changamoto, lakini fanya mambo ambayo wengine wanayakimbia, huko ndiko unakotakiwa kukimbilia ili kujenga mafanikio makubwa.
Angalia yale mambo ambayo hayawezekani, halafu amua kuyafanya wewe ukawa mtu wa kwanza kuyafanya mambo hayo. Usijali ukubwa wake, chukua hatua za kuhakikisha unayafanya na hili litakiusaidia kuyafanikisha.
Maisha yako utayabadilisha sana kwa kufanya yale mambo ambayo yanaogopwa na wengi na wewe ikiwa utaamua kuwa kinara kwa kuyafanya kwa kishindo chote na kwa uhakika mkubwa.  Ukiamua inawezekana, ‘do what cant be done.’
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote manakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.