google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 10, 2017

Jifunze Kuwekeza Mambo Haya Katika Maisha Yako.

No comments :
Ili uweze kuwa bora katika maisha yako huna budi kuwekeza mambo mbalimbali ambavyo nitayeleza katika makala haya, ambayo yatakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuwa bora.
Kama ambavyo mara kadhaa nimekuwa nikinukuliwa nikisema ya kwamba hatma maisha yako yapo mikononi mwako, hivyo jifunze ni kwa namna gani wewe binafsi utakuwa kiongozi wa maisha hayo, hata mwanafasafa mmoja wa kimataifa Mr Jim Rohn aliwahi kusema ya kwamba huwezi ukasema unataka kutengeneza mwili wako katika misingi ya mazoezi, kisha wewe ukaamua kumuajiri mtu aweze kufanya mazoezi hayo kwa niaba yako, kisha ukategemea mabadiliko yaweze kutokea kwako. Jim Rohn anasema mabadiliko ya aina hiyo hayapo.
Hivyo kila wakati kama unataka kufanya mazoezi ya mwili ni lazima uweze kufanya wewe mwenyewe, halikadhalika katika maisha yako ya kila siku ili uweze kuwa bora ni lazima uweze kufanya vitu wewe mwenyewe ili uweze kuwa bora zaidi, kwa watoto wa mjini wana msemo wao ambao unasema ni vyema ujifunze kupambana na hali yako.

Hii ikiwa na maana ya kwamba ili uweze kuwa bora ni lazima  uwekeze katika mambo yafutayo;-


1. Simamia vitu vyako kwa ustadi na makini sana.
Kusimamia vitu vyako katika ustadi wa hali ya juu pasipo kuambiwa na mtu na pasipo kusimamiwa na mtu mwingine. Watu wengi wanashindwa kufikia kilele cha mafanikio kwa sababu wamekuwa wamekeza muda mwingi katika kufanya kazi bila kuwekeza nguvu na juhudi za kutosha katika jambo hilo.
2. Kila wakati jifunze vitu vipya vitakavyokufanya kuwa bora zaidi.
Vitu hivyo vipya ni lazima uviweke katika matendo pia. Wanasema ya kwamba mambo yanabadilika hivyo ni lazima na wewe ujifunze kubadilika ili kuendana na kasi ya mabadiliko hayo. Daima ni lazima ukumbuke hicho unachokijua leo hakitakuwa na thamani baada ya miaka miwili ijayo, hivyo wekeza muda mwingi katika kujifunza vitu vipya.
3. Jifunze kupanga mipango mikakati ya maisha yako.
Maisha bila mipango ni sawa na bure, hivyo kwa kuwa wewe unajua ni nini ambacho unakitaka jitahidi sana kupanga fanya mipango na mikakati itayokusaidia kuwa bora. Yupo mwandishi mmoja jina limenitoka aliwahi sema usipojenga misingi ya maisha yako vizuri yupo mtu utamsaidia kujenga misingi ya  maisha yake.
Hivyo kila wakati ili uweze kuwa bora ni lazima uzingatie hayo ili uweze kuwa bora katika maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757 909 942,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.