google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 18, 2017

Kama Unataka Kufanikiwa, Fikiri Hivi Na Usifikiri Vile.

No comments :
Jiulize kila wakati ni kitu gani unachofikiri kwenye akili yako, je, unafikiri dunia iko tofauti na wewe na haina usawa? Kama unafikiri hivi ndivyo itakavyokuwa kwako.
Jiulize pia ni unafikiri huwezi kufanya mabadiliko yoyote na umekwama wewe ni mtu wa kushindwa tu? Kama unafikiri hivi ndivyo itakavyokuwa kwako .
Kipi unachokifikiri kwenye akili yako, je unafikiri ushindi na kuiona kila siku ni fursa kwako? kile unachokifikiri, ndivyo itakavyokuwa kwako.
Mawazo hayo unayoyaweka kwenye akili yako mara kwa mara ndiyo anayokupa matokea  ya mambo ya nje yanavyoonekana.

Ndio maana ni muhimu sana kuweka akilini kile ambacho unataka kikutokea katika maisha yako kuliko kile ambacho hukitaki.
Usije ukajishangaa umejikuta umekuwa ni mtu wa majanga sana kila kukicha kwa sababu tu aya akili yako kuweka vitu ambavyo huvitaki maishani mwako.
Kufikiri yale muhimu ni muhimu sana kwenye maisha yako. Kipi unachokifikiri sasa, kitu hicho kinaweza kutokea kwenye maisha yako.
Hii iko hivyo kwa sababu mawazo unayokuwa nayo yanakuwa yanakusukuma hata wewe kuweza kuchukua hatua za aina fulani.
Kwa hiyo kile unachokifikiri ndio kinakufanya uwe mtu wa namna fulani, eidha uwe mtu wa kuchukua hatua au uwe mtu wa kushindwa.
Hata hivyo uamuzi unabaki mikononi mwako ni wa kitu gani ambacho ukifikiri. Kama ukiwa utafikiri hovyo, ujue kabisa utavuna hovyo kwenye maisha yako pia.
Tambua tu chochote unachokifikiri kinaweza kuwa kweli kwako. Chocchote pia unachokiamini, hicho pia kinaweza kutokea kwenye maisha yako.
Sasa kwa nini ujitese na kuumiza maisha yako kwa kufikiri mambo ambayo kwako. inabidi ujifunze kutawala mawazo akili zako ili ziwaze mema ya maisha yako.
Huhitaji kusema mawazo yanakuja yenyewe  na unasema utayazuiaje? Hilo ni kweli lakini inabidi utafute mbinu za kuweza kukusaidia kuwa na mawazo chanya.
Mbinu mojawapo ni kukaa na watu chanya na kusoma vitu vya mafanikio karibu kila siku ili vikujengee ukomavu wa kuweza kufanikiwa.
Kama umeamua kwa dhati kufikia mafanikio yako, ni wakati pia umefika wa wewe kujaza fikra zako mambo chanya ya kimafanikio ili ufanikiwe zaidi.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.