google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 12, 2017

Uwekezaji wa Mafanikio Yako Ni lazima Ujikite Katika Misingi Hii.

No comments :
Katika sayari hii lipo jambo kubwa ambalo unatakiwa kulifahamu kila wakati katika maisha yako, jambo hilo si jingine bali lile jambo la kuhakikisha unawajibika mwenyewe kwa asilimia mia moja. Nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba kwa kila kitu ambacho unakifanya hakikisha ya kwamba unajituma vya kutosha.
Kujituma huku ni katika kuhakikisha unajitoa muhanga katika kuhakikisha unajitoa kikamilifu katika kuyasaka mafanikio hayo. kama ambavyo umeuchoka umaskini basi yachoke na maisha ambayo hayukupi furaha ya kweli.
Mara nyingi tunasema ya kwamba watu wengi hawana furaha ya kweli hii ni kwa sababu ya mambo makuu mawali, japo la kwamba watu wengi hawana furaha ya kweli hii ni kwa sababu hawafanyi vitu ambavyo hawavipendi, wanafanya ili mradi wasogeze siku.

Jambo la pili watu wengi hawana furaha katika maisha yao hii ni kwa sababu watu hao wamechaguliwa maisha ya kuishi na watu wengine. Kwa mfano wapo baadhi ya watu wanafanyakazi fulani eti kisa mtu fulani alimwambie afanye kitu hicho kwani kinalipa sana. Watu hao mara baada ya kuanza kufanya jambo hilo wamejikuta matokea ambayo waliyategemea hayapo tena.
Hii ina maana gani? Hii ina maana ya kwamba furaha ya kweli katika maisha ya mwanadamu inapatikana kwa kuhakikisha wewe mwenyewe ndiye ambaye unakuwa kiongozi maisha yako kwa asilimia mia moja huku jitahada za kweli zikifanyika katika kuhakikisha unafanya kitu ambacho unakipenda pia.
Na sifa kubwa za mtu ambaye anahitaji kuwa kiongozi katika maisha yake ni kuhakikisha ya kwamba anasimama kidete katika kupanga mipango na mikakati kabambe ya jinsi ambavyo anavyoweza kuishi ndoto zake.
Hivyo kwa kuwa una shauku kubwa ya kuweza kuisha ndoto zako huna budi kuhakikisha ya kwamba kitu ambacho unakihitaji kinatokana kwa asilimia kubwa na kiwango cha uwekezaji wako.
Kiwango hicho cha uwekezaji wako ni lazima kiwe ni cha kweli, mara zote haiwezekani ukapanda mahindi katika shamba lako huku ukitegemea ya kwamba uje uvune maharage. Na pia imeandikwa yeyote apandaye kwenye mawe asitegemee kuja kuvuna mavuno ambayo aliyatarajia.
Huenda nikawa nimekuacha njia panda pale niliposema ni lazima ufanye uwekezaji ukadhani namanisha pesa, hapana sina maana ya pesa bali maana yangu ni hii uwezezaji wa msaka mafanikio upo katika mambo yafutayo;
1. Jinsi mtu huyo anavyoipangilia ratiba yake kuanzia anapoamka hadi anapokwenda kulala. Mara nyingi ratiba za watu wengi kwa siku nzima huwa hazielewiki, kwa mfano wapo baadhi ya watu ukiwauliza hivi kwa siku nzima ya leo umefanya nini? Watu hao wanaweza wasiwe na majibu ya moja kwa moja ya kukupa, kwani wengi wao ratiba zao huwa hazipo katika mpangilio.
Hivyo kama wewe ni miongoni mwa watu hao ambao huwa hawana ratiba muhimu, unachotakiwa kufanya kuanzia sasa ni huhakikisha ya kwamba unatengeza ratiba ambayo itakuongoza wewe katika kufanya mambo mbalimbali ya muhimu. Endapo utaamua kufanya hivyo ambavyo nimekueleza basi tegemea matokea makubwa sana.
2. Uwekezaji wa msaka mafanikio ni lazima uwe katika misingi ya kuweka vipaumbele vya kiutendaji wa siku nzima. Huwezi kusema unataka kufanikiwa harafu ukawa huna vipaumbele ambavyo vitaongoza maisha yako kwa siku nzima. Vipaumbele hivi ni lazima viwe katika kujua ni nini ambacho utaanza kukifanya na nini kitafuata.
Endapo hutajijengea utaratibu huu wa kuweka vipaumbele katika maisha yako ni lazima ujue kabisa maisha yako yatakuwa katika misingi ya kujiua wewe mwenyewe. Hivyo kwa kuwa sasa ulichokisoma siku ya leo  umekielewa vyema ninachotaka kukusihi ni kwamba hakikisha ya hiki ulichokisoma unakiweka katika matendo.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni ndimi Afisa mipango wa mafanikio yako,
Benson Chonya,
Mawasiliano; +255 757 909 942,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.