google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 23, 2017

Jiandae Kwa Hiki Ili Kufanikiwa Katika Kila Jambo.

No comments :
Ili kuweza kufanikiwa katika jambo lolote kwenye maisha yako unahitaji kuwa na UJASIRI. Unahitaji kuwa na ujasiri wa kushinda hofu zako na pia unahitaji kuwa na ujasiri wa kushinda changamoto zozote zile zinazozojitokeza mbele yako.
Na ujasiri tunaouzungumza hapa hauji kwa bahati mbaya, ujasiri huo unakuja kutokana na maandalizi muhimu ambayo unatakiwa uyafanye. Hautaweza kuwa jasiri kama huna maandalizi ya muhimu kwako.
Inawezekana unaanza kujiuliza ujasiri huo utaujenga kwa vipi? Sikiliza, na twende kwa mfano. Mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa kusoma kabla ya mtihani, huyu anakuwa hana wasiwasi sana tofauti na  yule mwanafunzi ambaye hakusoma kabisa.
Halikadhalika wale wanaoongea mbele za watu alimaarufu ‘public speaker’ ambaye kabla ya kwenda kuongea usiku alifanya mazoezi, atakuwa ana ujasiri tofauti na yule ambaye hakuweza kufanya mazoezi na kuamua kwenda tu kuongea.

Hata katika maisha na mafanikio yako, unahitaji kuweka maandalizi ya nguvu ili kuwa na ujasiri na kufanikiwa. Maandalizi haya utayapata tu kwa wewe kuamua kufanya kazi kwa bidii na nguvu zote.
Kufanya kazi kwa juhudi na nguvu zote ndio kutakapokupa ujasiri wa kuweza kushinda hofu na kila aina ya woga ambao unakukabili.  Watu wote ambao hawana hofu sana katika maisha ukiwatazama vizuri  ni wachapakazi.
Ni wazi tu, hofu hiyo wanakuwa hawana na badala yake wanakuwa ni majasiri, unajua ni kwa sababu gani, ni kwa sababu wanakuwa wanajua hata mambo yagome vipi kwao hakuna kitu kitakachoweza kuharibika kwao.
Si jambo la kujiuliza sana unapokuwa unashindwa kuwajibika au kuchapa kazi kwa juhudi sana elewa tu kwa namna yoyote utaanza kukosa ujasiri na mwisho wa siku woga mwingi wa maisha yako utaanza kukuvaa.
Fanya wajibu wako. Fanya kazi kwa bidii sana bila kujali kazi unayoifanya ni ya aina gani na kwa kufanya kazi kwako huko utajikuta ukiwa ni mtu ambaye unavuta mafanikio kwa kiasi kikubwa sana kama sumaku.
Ujasiri ni kitu cha muhimu sana katika mafanikio yoyote yale. Kumbuka kama nilivyoanza kwa kusema bila kuwa na ujasiri huwezi kufanikiwa hata ufanyaje, zaidi utaendelea kubakia na maisha yako hayo.
Kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.

Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO na KIENYEJI ASILIA. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na bei kwa kila kifaranga ni tsh. 1800/=. Wote mnakaribishwa.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.