google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 30, 2017

Kama Utazingatia Hatua Na Mawazo Haya, Tayari Umefanikiwa.

No comments :
Siku zote ieleweke hivi, kama unarudia mawazo yako, kama unarudia hatua fulani hivi mara kwa mara ni wazi utakuwa bora sana kwa hicho unachokirudia kila wakati.
Haijalishi kitu gani unachokirudia sana kwenye mawazo yako yaani unakifikiria sana ila kitu hicho kitakuwa sehemu ya maisha yako kama utafanya hivyo sana.
Haijalishi ni hatua zipi utakuwa unazirudia sana kwenye maisha yako ila hatua hizo zitakua matokeo ya kitu fulani hivi kwenye maisha yako.
Ikiwa utatenga muda na masaa kadhaa kwa wiki kufikiria na kutenda jambo lolote lile katika maisha yako, uwe na uhakika jambo hilo utalivuna.

Kwa mfano, ukiona una maisha mabovu au una maisha mazuri ujue ni mwendelezo wa mawazo fulani ambayo ulikuwa nayo kwa siku za nyuma.
Mawazo yapi uliyonayo kwa muda mrefu, ni hatua zipi ulizonazo kwa muda mrefu hizo ndio hatua zinazokupa matokeo ya kitu fulani kwenye maisha yako.
Hauhitaji sana kumtafuta mtu pengine anayefanya maisha yako mabaya, kama iko hivyo kweli, ila unachotakiwa kufanya ni kukagua hatua na mfumo wa mawazo yako ukoje.
Wakimbiaji wote duniani  wanaelewa vyema kabla hujawa mshindi katika mbio lazima ufanye mazoezi mengi sana yatakayokufanya uwe mshindi.
Kuna wakati itakutaka ukimbie mbio za muda mrefu zaidi ya mashindano unayochukua na tena mara kwa mara hadi uweze kushinda.
Kuwa mshindi katika mbio kwa wakiambiaji wanajua kabisa sio swala la mara moja bali ni swala linalochukua mazoezi karibu ya kila siku.
Halikadhalika, hata washindi katika maisha ni watu ambao wanajuhudi endelevu  za kila siku kwenye maisha yao. Kitu hiki leo kikikataa kuna kingine kitafanyika hadi kieleweke.
Hivyo hata kwako inatakiwa ieleweke mawazo yanayojirudia mara kwa mara akili mwako, hatua zinazojirudia hizo ndizo zinazokupa mafanikio yako.
Mafanikio yako yanajengwa hatua kwa hatua, unatakiwa kujua hata kama hatua unazo chukua ni kidogo lakini hatua hizo zipo na ipo siku zitakufanikisha.
Una uwezo wa kufanya maisha yako kuwa bora zaidi ikiwa utakuwa na mawazo na hatua bora zinajirudia akilini mwako kila wakati.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.