google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 16, 2017

Mambo Yako Yanapokuwa Hovyo Kabisa…Fanya Hivi.

No comments :
Inapofika mahali kwenye maisha yako unaona kila kitu ulichokifanya hakijafanikiwa na unaona kabisa umepoteza muda mwingi kwa kufanya kazi ya bure, unapokutana na kipindi hiki hapa inatakiwa ujifunze kutulia sana.
Katika kipindi hiki, hutakiwi kukurupuka  na kuchukua hatua za haraka ambazo hatua hizo lengo lake litakuwa kama ni kufidia pale ulipodondoka au pale ambapo hujafanikisha.  Unatakiwa kutilia kwa kuliza akili yako sana.
Kama utataka kukurupuka na kuchukua hatua za haraka , hazitakusaidia sana kwa maana kichwa chako kitakuwa na haraka sana ya kuwaza kukamilisha mambo yako, hivyo hakuna hata thamani kubwa utakayoweza kuitoa.
Hiyo inamaanisha nini, unapoona mambo yamekwenda hovyo, mambo hayaeleweki, usije juu sana, tuliza akili yako, weka nguvu za uzingativu eneo moja kwanza kutaka kubadilisha kitu kimoja na hayo mambo mengine utayabadlisha pia.


Lakini ikiwa utaamua kukurupuka na kuchukua hatua zote unazozijua za kufanya maamuzi ya zimamoto, elewa kabisa utakuwa ni sawa na mtu ambaye ameamua kuongeza ‘petroli’ kwenye moto, hakuna utakachokifanikisha.
Kuna wakati unaweza ukaanguka kwenye maisha, kwa sababu ya maamuzi kama haya ya kukurupuka hasa mara baada ya kugundua kwamba mambo yako hayaja kwenda sawa kama wao wanavyofikiri au kama wao wanavyotaka.
Huhitaji kuwa na wasiwasi mwingi, unahitaji kutulia, hebu jiulize hapa, ukiwa una wasiwasi kwa sababu ya mambo yako kwenda hovyo hiyo kwako itakusaidia kitu gani? mpaka hapo umejua ambacho unapaswa kuwa nacho ni utulivu.
Uwezo wako wa kutulia ndio utakaokusaidia sana kuweza kufanya mambo kwa busara na umakini mkubwa utakaoweza kupeleka wewe kutoa thamani inayotakiwa, kinyume cha hapo utakuwa unajidanganya.
Kwa hiyo, kama unaona mambo yako yamekwenda hovyo, jambo la makini sana unalotakiwa kulielewa hapa na kulifanyia kazi wewe ni kutuliza akili yako kama tulivyoanza kusema mwanzoni mwa makala haya.
Akili yako inapotulia utashangaa changamoto zako utakuwa unazivuka kwa jinsi unavyotaka wewe. Hakuna kinachoshindikana hasa kunapokuwa na utulivu. Utulivu ni kitu cha msingi katika kuweza kukusaidia kufanikisha ndoto zako muhimu ambazo hata ulikuwa unaona hazifanikiwi tena.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.