google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 3, 2018

Chunga Sana Matumizi Haya Ya Pesa Ili Yasikupoteze.

No comments :
Kitu cha msingi unachotakiwa kuzingatia wakati unatumia pesa zako, ni ubora wa vile vitu ambavyo unakwenda kuvipata wakati unatumia pesa zako.
Kama unatumia pesa zako kwa vile vitu ambavyo viko bora wakati wote, basi pesa zako wakati wote ziko salama na zitakusadia kupiga hatua ya aina fulani.
Kama unatumia pesa zako kwa mambo ya hovyo hovyo basi hata kama kipato chako ni kikubwa kiasi gani, pesa hizo utakuwa unazipoteza tu bure na hakuna unachofaidi.
Wakati wote unatakiwa kuzingatia ni kwa namna gani unafanya matumizi yako kwa ubora, ikiwa unafanya matumizi yako kwa ubora utajiweka kwenye wakati bora pia.
Watu wengi wanajikuta wameishia na hawana kitu kwa sababu ya kufanya matumizi yasiyo ya msingi, bali wanafanya matumizi ya kuwabomoa.
Kila wakati chunga matumizi yako na hakikisha unajua pesa zako zinakwenda wapi kila siku iitwapo leo.

Kutumia zako hovyo, huko ni kujitakia majanga yaw ewe kuweza kuishia kwa baade. Tumia pesa zako kwa busara nazo pia zitakulinda.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.