google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 1, 2018

Jinsi Unavyotakiwa Kuishi Katika Mwaka Huu Wa 2018 Ili Uweze Kufanikiwa Katika Maisha Yako.

No comments :
Ndugu rafiki katika mafanikio,  awali ya yote ni kutakie heri ya kuona mwaka mpya. Lakini nitakuwa mchoyo wa wafadhira kama nitashindwa kumshukuru Mungu ambaye ndiye kasababisha hayo yote yaweze kutokea.
Lengo la kukuandikia makala haya kwako ni kukumbusha ya kwamba mwaka ndio huo umeanza, hivyo natamani sana na wewe mwenzangu ufanikiwe katika maisha yako kama ambavyo mimi binafsi nimepiga hatua kwa kiwango fulani.
Hivyo kwa kuweza ili uweze kupiga hatua hizo vyema ukayatazama mambo yale ambayo yapo mbele yako katika mwako huu, kwani yaliyopita si ndwele tugange yajayo, hajalishi ni mangapi umepitia kipindi cha nyuma.
Lakini pia katika mwaka huu wa 2018 unahitaji kuwa na marafiki wanakukosoa kuliko wale wanakusifia tu. Marafiki wanakukosa watakupa mwanga na akili mpya ya kufikiri na kuweza kutenda jambo fulani kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Jambo hilo ni la muhimu kwa sababu wakati mwingine ukikosa watu wanaokukosoa kunakufanya ushindwe kuwa mbunifu katika mambo mbalimbali ambayo unayafanya kwenye maisha yako ya kila siku.
Pia hiyo haitoshi kwa mwaka huu wa 2018 ili uwe wa mafanikio, unalazimika sana kufanya haya ili yakusaidie kuweza kupiga hatua, ikiwa utakwenda kinyume ujue kuna namna fulani hivi, utaweza kukwama.
1. Piga kazi sana. Hapa kama inawezekana ukajikana kabisa jikane, ila chapa kazi hadi uweze kuona mafanikio yako yakitokea na kuwa wazi. Kazi ndio msingi wa maendeleo yako hata kama mfukoni huna ktu kabisa.
2. Jifunze. Kubali kuifanya 2018 uwe mwaka wa kujifunza kwako. jifunze kupitia vitabu, jifunze kupitia kwa wengine pia. Ukikwama kujifunza utaendelea kushindwa kama ambavyo miaka mingine umekuwa ukishindwa pia.
3. Jenga nidhamu kubwa. Kazana kwa mwaka huu, kujenga nidhamu tena na tena kwenye kila eneo la maisha. Jenga nidhamu ya pesa. jenga nidhamu itakayokusaidia kuweza kutimiza ndoto zako za kila siku.
4. Usipoteze muda. Jenga historia kwa 2018 usikubali kupoteza muda wako tena. Kila unachokifanya, hakikisha unakifanya kwa mahesabu ytakayoweza kukuokolea muda wako. Kama wewe utazidi kupoteza muda utakwama pia.
5. Kuza mahusiano bora na wengine. Hakuna mafanikio yanayojengwa ukiwa peke yako. Jitahidi sana kukuza  mahusiano bora ili yakupe mafanikio. Ukishirikiana na wengine utaweza kufikia mafanikio yako.
6. Timiza lengo lako kubwa moja. Usikubali 2018 ikakupita bila kutimiza lengo lako moja kubwa. Hakikisha kuna lengo lako moja kubwa unalitimiza, hata kama yapo mengi ila lengo lako moja kubwa litimize.
Ni matumaini yangu makubwa mapendekezo yangu utayafanyia kazi na kuyatekeza.
Nikutakie siku kuu njema na sherekea kwa amani kubwa.
Ni wako katika mafanikio, Benson chonya.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.