google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 28, 2018

KIPAJI CHAKO; Wosia Wa Mafanikio Kutoka Kwa Mama, Sehemu Ya 02

No comments :
Ilipoishia wiki iliyopita
“Mama Ester mke wangu kwa kweli mimi hali yangu siku ya leo naona haipo sawa kabisa hivyo sidhani kama nitapona mke wangu ” sauti ile ya baba yenye kila aina zote  upole na ukarimu zilinifanya niamini ya kwamba baba alikuwa amezidiwa sana usiku ule.
Sasa endelea nayo………
Kwanini unasema hivyo Baba ester? Mama naye alihoji.
“Kwa kweli mke wangu hali yangu ni mbaya sana, najisikia joto sana harafu na kifua changu kinawaka moto hivyo nakuomba uchukue japo nguo unipepee mke wangu”

Pamoja hali ya baridi iliyokuwepo usiku ule, nilishangaa kwanini baba alikuwa anahisi joto?
Huku nikiwa nimesimamisha masikio yangu yalikuwa yamesimama dede kama mnala wa baberi kusikiliza kile kilichojili chumbani kwa wazazi wangu,
Kwa wakati huo waoga ndio uliokuwa umetawala akili mwangu……..
Nikiwa nikiendelea kusikiliza kile kilichokuwa kikijili chumbani kwa wazazi wangu, nilimsikia mama akinyanyuka na kwenda kufanya kile baba alichomuagiza, japo na yeye mama yangu alikuwa ni mjamzito si ujauzito tu, bali ulikuwa ni ujauzito wa miezi saba na nusu.
Wakati maongezi ya baba na mama yakiendelea chumbani, nami huku nilikuwa nasali kwa kasi zaidi ya 4G ili mwenyezi Mungu aweze kumponya baba yangu, kwani yeye ndiye aliyekuwa msaada mkubwa sana katika familia yetu na masomo yangu kwa ujumla.
Wakati nikiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kumsaidia baba yangu aweze kupona haraka, nilimsikia baba akisema;
“mke wangu naomba unisamehe sana!” mama alihoji kwa sauti ya chini
“nikusamehe kwa lipi tena mume wangu?
Naomba unisamehe kwa sababu enzi za uzima wangu sikutaka kabisa kukufundisha kufanya biashara yeyote, zaidi ya kukufundisha kulima, japo ilikuwa ni kwa asilimia chache sana  na kama unavyojua ya kwamba kwa hapa kijini kwetu kitu pekee ambacho hutufanya sisi kupeleka mkono kinywani ni kilimo pamoja na biashara ambayo nilikuwa naifanya mimi pekee yangu pasipo kukufundisha wewe.
Na siku ya leo kifo kinanikabiri na nikikutazama nagundua nakuacha katika mateso makali sana, kwani nakucha pasipo kukuachia ujuzi wowote ambao utakusaidia katika kufanya biashara, lakini pia nasononeka kwani najua familia yangu itaishi maisha magumu sana.
Lakini jambo la mwisho nawaza juu ya ujauzito ulionao kwani nafahamu fika mwanagu atakua bila kujua sura ya mimi baba yake......
Wakati baba anaendelea kusema maneno yale nilijawa na simanzi mayoni....... Niliwaza ndani ya nafsi yangu, ni kwanini baba alisema maneno yale? Wakati baba akiendelea kuzungumza na mama, nilimsikia baba sauti ikizidi kufifia huku akizidi kuongea kwa tabu.
Mmmmmke wangu, nananaku.......pe........nda sana, nakuomba nawe umpende mwaaaaanangu Ester pamoja na huyo Mmm____mmtoto wetu mwingine ambaye atazaliwa.
Mara baada ya baba kusema maneno hayo sikuisikia tena sauti ya baba zaidi ya kuisikia sauti ya mama, ikisema;
Baba Ester........ Bababa ester........
Mume wangu baba ester.......amka mume wangu...........
Baba Ester tafadhari nakuomba uamke mume wangu
Niliendelea kumsikia mama akimuita baba pasipo mafanikio. Wakati kule chumbani kwangu nikiwa katika hali ya ulutivu, nilimsikia mama akiniita kwa sauti ya juu,Ester mwanangu njooooo.
Sauti ile ya mama ilinifanya niogope, kwani ilikuwa si sauti ya kawaida ambayo mimi binafsi nilikuwa nimeizoea, nilikaa kimya kidogo pasipo kuitika, mama alirudia kunita tena kwa sauti nyingine.
Ester mwanagu njooo, baba ako anaku……..
Nilitoka mbio chumbani kwangu hadi chumbani kwa kina mama ambapo sauti ya mama ilinita huko. Nilifika mlangoni wa chumba cha wazazi wangu na kubisha hodi,,,,,,, hooo kabla sijamalizia kusema hodi, mama aliniamulu nipite.
Je ni nini ester alikikuta huko chumbani, usikose muendelezo wa hadithi hii nzuri ya kusimumua sehemu ya tatu siku ya jumamosi ijayo.
Mtunzi: Benson chonya
0757909942



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.