google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 30, 2018

Vitu Vya Kufanyia Kazi Sana Katika Maisha Yako Ya Mafanikio.

No comments :
Yapo mambo mengi sana ya kufanyia kazi katika safari ya mafanikio ili uweze kupiga hatua. Kwa bahati nzuri sana mambo hayo tumekuwa tukijifunza hapa DIRA YA MAFANIKIO karibu kila siku, naamini hilo unalijua vyema.

Leo hii kupitia makala haya, tumekuandalia vitu vingine vya msingi vya kufanyia kazi sana katika safari yako ya maisha ya mafanikio. Soma kwa makini na kutendea kazi, na maisha yako utayabadili ikiwa utachukua hatua.

1. Njia ya mafanikio ni njia ambayo ina changamoto nyingi sana katikati yake. Pale tu unapoanza safari yako ya mafanikio kwa chochote kile unachotaka kukifanya elewa mbele yako kuna changamoto tayari zinakusubiri. Huwezi kukwepa changamoto.
2. Ikiwa utakosa nidhamu kwenye maisha yako, basi dunia itakuonyesha jinsi nidhamu inavyotakiwa iwe. Utapewa adhabu kulingana na kukosa kwako huko nidhamu. Matokeo yoyote utakayoyapata maishani kwa sababu ya kukosa nidhamu usilaumu.
3. Jiruhusu mwenyewe katika siku hii ya leo uishi kwa kutoa thamani yote uliyonayo. Usiishi nusu nusu kwa kuwaza mambo ya jana au juzi. Usiishi nusu nusu kwa kufikiria kwamba kesho itakuwaje, ishi leo kwa siku nzima kama ilivyo ili kupata matokeo bora.

4. Kila mafanikio ambayo umeyapata, ni matokeo ya kwamba kuna vitu ambavyo ulivifanya na vikakupa mafanikio hayo. Kwa kujua hilo, endelea kufanya vitu hivyo, endelea kuchukua hatua ili upate mafanikio mengine zaidi na zaidi tena.
5. Maisha yako yanaishia wapi au yatafika wapi, inategemea sana na vitu viwili ambavyo ni mtazamo na jinsi unavyochukulia mambo. Mtazamo wako na jinsi unavyochukulia mambo ndivyo vinavyoamua maisha yako yaweje.
6. Chochote unachokizingatia kwenye maisha, kitu hicho kinakua. Kama unasahau kuzingatia kile kinachokupa matokeo ya kubadili maisha yako, hiyo itakuwa ni kazi bure hata kama ungekua unatunza muda vizuri sana. Anza leo kuzingatia sana kile kinachobadili matokeo ya maisha yako na utafika mbali kimafanikio.
8. Miaka kumi ijayo kuanzia leo ikifika, haitajali ulivaa kwa sasa kiatu cha aina gani au ulivaa nguo za mtindo upi zilizotoka au ulitembelea sana maeneo yapi au uliangalia ‘movie’ ipi nzuri kwako. Miaka hiyo kumi ijayo itajali na itakuja na matokeo ya ulichowekeza leo, bila kujali uliwekeza kitu cha aina gani.
9. Usijaribu kuangalia nyuma kwenye maisha yako na kuchunguza yale maeneo kila wakati uliyokwama na kujiona huwezi kitu. Ni vyema kuangalia maeneo uliyofanya vizuri na kuedelea kujiboresha na hadi kuweza kufanikiwa zaidi ya hapo.
10. Moja ya tabia ambayo unatakiwa kuiendeleza ndani mwako na katika maisha yako kwa ujumla, ni kwa wewe kutokuruhusu, kuwahukumu watu wengine. Usiumize kichwa chako sana kuwahukumu watu wengine, utapotea. Waache waishi maisha yao. Kuwahukumu watu mara kwa mara inaweza hata ikakuletea msongo wa mawazo.
11. Kila mtu unayekutana naye kuna vitu vitatu ambavyo anavyo ndani yake;-
 Kuna kitu anachokipenda.
 Kuna kitu anachokiogopa.
 Kuna kitu ambacho amekipoteza.
12. Watu wengi katika maisha hawasikilizi ili kuelewa, bali wanasikiliza ili kukimbilia kujibu. Kuwa msikivu mzuri unapoongea na watu wengine, hiyo itakusaidia sana kudumisha mawasiliano yako na kwa bora kabisa.
13. Katika hii dunia, hakuna kitu ambacho kinaitwa ulinzi bali kuna fursa. Kama unafanya kazi na kutegemea sana ulinzi au ‘security’ kama wengi wanavyodai unajipoteza. Tafuta fursa za kukusaidia kufanikiwa na si kutafuta ulinzi.
14. Siri ya kuweza kusonga mbele kwa chochote kile unachokifanya ni kuanza. Usijidanganye sana kama unapiga hatua mbele kama hujaanza. Ni muhimu sana kuanza, kwani unapoanza unajenga ‘momentum’ ya kukusaidia kuweza kusonga mbele zaidi kila siku kuliko usingeanza kabisa.
15. Kupata utajiri ni zaidi ya mawazo na mipango uliyonayo. Ili uwe tajiri ni lazima uwe na akili ya kitajiri/rich mindset na sio mawazo na mipango peke yake. Mawazo mazuri na mipingo mizuri haiwezi kukusaidia kama una ‘poor mind set.’
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.