google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 2, 2018

Usitoe Chozi Kwenye Maisha Yako, Kwa Sababu Hii.

No comments :
Kama kuna wakati unaona maisha yanakuchanganya hasa kutokana na changamoto unazokutana nazo, usije ukakubali ukafanya kosa la kuchanganywa huko, badala yake tuliza akili yako na tafuta mwelekeo sahihi wa maisha yako kwa kuweka mambo sawa.
Ikiwa unaona pia unaweka juhudi nyingi sana na juhudi hizo hazikupi matunda sahihi, hapa tena usikatishwe tamaa, endelea kuweka juhudi, lakini tafuta kuelewa kwa nini juhudi zako hazikufanikishi na anza kutafuta njia nyingine itakayokupa matokeo makubwa kwako na kuweka mambo sawa.
Upo wakati katika maisha yako ambapo kuna mtu au watu  watakurudisha nyuma hata bila ya wewe kutegemea. Inapotokea wakati kama huu, sio suala la kutupa lawana na kusikitika, bali ni kuuvaa ujasiri na ushujaa na kutafuta mwelekeo upya kwa kuweka mambo yako sawa.
Kuna wakati katika  maisha yako unajiona upo njia panda, huelewi hata ufanye nini, inapofika wakati huu , jifunze kuweka nguvu za uzingativu katika kitu kimoja na kutafuta mwelekeo sahihi utakaokusaidia kuweka mambo yako sawa na yakae katika mkao wa mafanikio.
Zipo nguvu nyingi na kubwa sana katika maisha yako, ambapo nguvu hizo zina uwezo wa kubali hali yoyote ambayo unayo na unaona ni  mbaya na nguvu hizo hadi kukupa mafanikio halisi kama vile unavyotaka iwe.
Ndio maana, badala ya kulalamika na kutoa kila aina ya visingizio, jitahidi sana kuweka mambo yako sawa, kila unapoweka juhudi ya kuweka mambo yako sawa, utajifunza na kugundua kwamba kumbe unaweza ukatawala maisha yako kwa jinsi unavyotaka.
Je, katika maisha yako kuna kipi ambacho unakiona ndio tena basi kimeharibika na hakiwezi kukusaidia hata kufanikiwa. Kama kipo kitu cha namna hiyo, anza kikiweka sawa na kutafuta njia ya itakayofanya kitu hicho kikupe matunda uyatakayo.
Hata mambo yko yakae hovyo vipi, unapaswa kuelewa upo wakati yataweza yaka kaa sawa na kuwa bora kabisa. hupaswi kuchanganikiwa na maisha yako. unapaswa kuweka sawa maisha yako.
Ukiona unaanza kuchanganyikiwa kwa sababu ya maisha, oooh kaa mkao wa kula, utakuwa unajipoteza rafiki yangu. Kila wakati rudi kwenye njia kuu ya mafanikio kwa kuhakikisha unaweka mambo yanakuwa sawa.
Dunia hii haikutaki wewe uendelee kulia lia, dunia hii inakutaka uendelee kuwa mbishi tena mbishi haswaa ili uweze kutoboa kimafanikio, kinyume cha hapo mateso makubwa yatendelea kukuandama pasipo kuchoka.
Kitu unachapaswa kukizingatia au kutoka nacho leo hii kupitia makla haya ni kwamba, usichanganywe na maisha na wewe ukakubali kuchanganyika. Usivurugwe na wewe ukakubali kuvurugika, tafadhari rudi kwenye njia kuu.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.