google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 8, 2018

Misingi Ya Maisha Na Mafanikio Kutoka Kwenye Kitabu Cha The Top 200 Secrets Of Success And The Pillars Of Self-Mastery.

No comments :
Hiki ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi Robin Sharma  kwa malengo ya kuonyesha sheria na kanuni mbalimbali za maisha ambazo inatakiwa kuzisimamia na kuzifanyia kazi kila siku kwenye maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.
Ni kitabu kifupi ambacho ukikazana kukisoma ni rahisi tu kukimaliza kwa siku moja, kwani ni kitabu ambacho hakina maelezo marefu sana na yapo mambo mengi ya kujifunza lakini, yafuatayo ni baadhi ya machache yake.
1. Tenga jumapili moja kila wiki, halafu tafuta muda ambapo kila jioni unakuwa unakaa angalau saa moja na kuanza kutafakari juu ya maisha yako wapi unapotoka na wapi unapokwenda na kisha kupanga mipango ya wiki linalofuata. Tabia hii ukiisimamia kiuhakika, itakufanya upige hatua sana.
2. Kaa karibu na watu ambao utaamua kujifunza vitu kutoka kwao. Usikae na watu ambao wanaweza kukuzamisha kimaisha, watu hao ni hatari sana kwenye maisha yako kimafanikio na ni rahisi kukurudisha nyuma.

3. Usiende kitandani kulala ukiwa na kazi yoyote ya kufanya au kuna jambo la kina la kulifikiria. Kitandani pako pafanye iwe ndio sehemu ya wewe kwenda kupumzika, ukienda kulala, na ulale kweli kama mtoto mdogo mdogo.
4. Usijaribu kula masaa matatu kabla hujalala. Kiafya, inashauriwa kula masaa zaidi ya matatu kwa sababu hiyo inakuwa inapelekea mwili wako unafanya mmeng’enyo bora wa chakula, kinyume na ukila ndani ya saa tatu na ukalala, unaharibu afya yako.      
5. Kila siku fanya mambo makubwa mawili ambayo kikawaida hupendi kuyafanya. Kwa kufanya mambo hayo mawili, inakusaidia kujenga sfa za ushupavu wa kufanya mambo mengine tena zaidi na zaidi yatakayokuweka kwenye ngazi kubwa ya mafanikio.
6. Furaha ya kweli ndani yako inakuja, mara baada ya wewe kuweza kutimiza malengo yako. Ukishatimiza malengo yako ile furaha ya kweli inajengeka ndani yako kwa kiasi kikubwa sana, haijalishi yawe malengo yako binafsi au malengo mengine ya kawaida.
7. Kila siku unapochagua kufanya kitu au unapochagua kufanya jambo la aina fulani, unatakiwa kwenda hatua ya ziada. Usijjichangamnye ukafanye na ukaishia pale tu, nenda hatua ya ziada na hapo utakuwa unatengeneza mafanikio makubwa sana kwa upande wako wakati wote.
8. Lala kidogo kwa wastani, tumia kidogo matumizi yako na fanya kazi kwa nguvu sana, na mafanikio utayaona kwa upande wako.
9. Usiruhusu kujadili mipango ya maendeleo yako binafsi na watu wengine. Unachotakiwa kufanya ni kuwaacha watu hao waone MATOKEO na si MCHAHAKATO wa kila hatua unayopitia. Kujadili  mipango ya maendeleo yako binafsi na watu wengine, huko ni kujianika sana na kujiruhusu ujulikane kwa uwazi bila sababu.
10. Vitu vinagunduliwa kwa namna mbili tu. Kwanza, kwenye akili yako na pia ni nje katika umbo la kawaida. Kwa mfano; nyumba inaanza kujengwa kwenye karatasi kwanza, halafu unakuja kuiona nje ikiwa nyumba halisi ikionekana.
Chukua hatua kila siku kujifunza haya muhimu uliyojifunza.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.