google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 14, 2018

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Anayekata Poli, Moshi Utaonyesha Tu.

No comments :
Ni wakati mwema na siku njema ambayo tunakutana tena katika jamvi letu pana la kuweza kujifunza hekima za maisha na mafanikio. Hapa kama ambavyo nimekua nikukueleza tunakuwa tunajifunza misemo ambayo inabadilisha maisha yetu.
Misemo hii ni ipi kama wewe ni mgeni hapa, hii ni misemo ambayo ilitolewa na babu zetu enzi hizo ambazo wewe hukuwepo lakini ina maana sana katika kujifunza kwetu, ndio maana tunaiita hekima za maisha na mafanikio.
Kwa upande wangu kama upo mbali nakualika, sogea karibu jamvini, sogea na kalamu yako ili tuweze kujifunza hekima za maisha na mafanikio kama ilivyo ada yetu kwa siku kama ya leo. Karibu sana tujifunze pamoja;-

1. Anayekata poli, moshi utaonyesha tu.
Kwa kawaida kama mtu yuko polini na amekazana kukata msitu au poli, haina haja ya kusema sana kwamba mtu huyo anafanya kitu gani, hata kama hujaambiwa yaani uko mbali utakachosikia ni sauti ya shoka na moshi unaofuka baada ya miti kuchomwa.
Kupitia hekima hii ya mafanikio inatupa fundisho kwamba; kama kuna kazi inafanyika hauna haja ya kuiongelea sana kazi yako hiyo, mafanikio yenyewe yataonekana tu kwa nje bila ya wasiwasi. Hio ni sawa na kupiga kazi kimya kimya lakini matokeo tutayaona.
Kwa mantiki hiyo iko hivi, kama kuna kazi unaifanya, ifanye tena kwa nguvu zote, usitake kuwaonyesha watu kwamba ni matokeo yapi yatatokea, hayo matokeo yatatoka tu hata kama usiposema kwani tunaambiwa mkata poli moshi utaonyesha tu na hakuna ubishi.
Mtu anaweza asione unachofanya, hilo lisikusumbue wala kukuumiza akili, wewe piga kazi, fanya unachofanya kwa uhakika, unaweza ukawa kwenye hatua za kama kupanda mbegu tu hakuna kinachoonekana, lakini matokeo yatakuja.
Itafika muda au wakati watu wataanza kuona moshi, na hapo ndio watagundua alaa kumbe kulikuwa kuna mtu yupo msituni anakata poli. Na kwa bahat nzuri moshi huo utaonekana mpaka mbali, hivyo piga kazi usife moyo, moshi utaonekana tu wa mafanikio yako.
2. Yule anaemulika nyoka usiku na tochi, huanzia miguuni mwake.
Ni kawaida sana usiku unapaoambiwa kwamba kuna nyoka hapo hatua ya kwanza ambayo unachukua kama una tochi ni kuanza kumulika miguuni mwako. Hilo wewe unaweza kulifanya hivyo na mwingine anaweza kulifanya hivyo pia.
Hekima hii ina maana gani kwetu, ni kwamba, ni vyema kabla hujatatua changamoto za wengine au kabla hujaangalia matatizo ya wengine walionayo na kuanza kuwalaumu pengine ni bora ukaanza kujiangalia kwanza wewe, je, uko sawa.
Ni rahisi kuwakosoa wengine kumbe wewe ndio umeisha kabisa na ndio unatakiwa kukosolewa wa kwanza. Hili ni onyo linalotutaka kushugulika kwanza na sisi na kujijua vizuri na kisha kutoa msaada kwa wengine.
Unaweza ukawa unamulika nyoka mbele na matokeo yake ukang’atwa wewe na ndivyo ilivyo kwenye maisha unaweza ukawa unashugulika na wengine na kujisau wewe. Kitu cha kwanza cha kuelewa hapa usijisahau anza kushughulika na wewe kwanza.
Unapogundua umemaliza kushughulika na wewe, kisha wafate wengine kuwapa unachotaka kuwapa ndio maana tunaambiwa yule anayemulika nyoka huanzia miguuni mwake na si vinginevyo, lazima uanzie pale ulipo.
Mpaka hapo kwenye hekima za maisha na mafanikio sina la ziada, tukutane wiki lijalo na wakati kama huu tena, tchaooo.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.