google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 15, 2018

Kama Utashindwa Kuangalia Matokeo Haya, Huwezi Kunikiwa Hata Kidogo.

No comments :
Yapo mambo mengi sana tunatoweza kuyapata kwenye maisha kila siku na tusijue chanzo chake nini. Kwa mfano, unaweza ukashangaa una maisha ya hovyo sana na hata usijue sababu yake hasa, basi tu unaishia kusema mimi ndivyo nilivyopangiwa.
Ukiangalia katika uhalisia wa ndani,  ni nani wa kukupangia maisha yako yakawa ya hovyo au ni kweli kwamba wewe una mikosi kama ambavyo unasema, kimsingi yote hayo unayoyasema unajidanganya tena mchana kweupe.
Kiuhalisia kunakuwa na chanzo, ambacho kinafanya maisha yako yawe hivyo yalivyo iwe mazuri au mabaya. Na chanzo hicho kwa bahati mbaya au nzuri kinaanzia ndani mwako wewe, yaani chanzo hicho kinakufanya uwe na maisha hovyo au mazuri.

Naona unanishangaa sana na kuanza kutafuta sababu za kujitetea kwamba, sasa iweje mimi nisababishe maisha yangu mwenyewe yakawa ya hovyo? Yaaa, inawezekana tu, ikiwa utashindwa kuangalia matokeo yanayosababishwa na mawazo na matendo yako.
Kila mara utajikuta ni mtu wa kuanguka sana, utakuwa unaanza jambo, lakini kabla hujafika kule linakotaka kufika ili likupe mafanikio, unashangaa tena umeshashindwa, unasimama tena kuanza kingine tena unashindwa.
Unapokuja kuangalia kwa umakini kwa nini wewe uko hivyo unakuja kugundua ni matokeo ya wewe kushindwa kuwa mwangalifu na matokeo yanayotokana na mawazo na matendo yako ya kila siku, hapo tu ndipo unapokwama.
Inabidi tukubaline ili ufanikiwe, Kila kitu unachokwenda kukifanya kwenye maisha yako  unapaswa kuangalia matokeo yake kwanza. Uelewe tu kwamba kila kitu unachokifanya kina matokeo yanaweza yakawa ni matokeo ya kukufanikisha au kukufanya ushindwe.
Na matokeo hayo kwa bahati mbaya au nzuri huwa hayatokei sasa hivi, yanakuja kutokea kwa baadae hata miaka kumi mbeleni, lakini yanakuwa ni matokeo ambayo yanatokana na mambo fulani hivi uliyoyafanya zamani kwa kipindi cha nyuma.
Matokeo utakayoyapata yanawezea kutokana na mawazo yako au hata vitendo vyako. Mawazo yako ya aina fulani hivi, yanaweza kukuzalishia matokeo ambayo unataka au huyataki, halikadhalika na vitendo vyako hivyo hivyo, vinaweza kukupa matokeo.
Kupata matokeo hayo yawe mazuri au mabaya, yote hiyo inategemea sana na kesho yako wewe unataka iweje. Ikiwa unataka kesho yako iwe bora, basi uwe na uhakika utakuwa makini sana na mawazo na vitendo unavyochukua kwa sasa.
Haitawezekana hata kidogo uwe na mawazo ya hovyo na vitendo vya hovyo wakati unatengeneza maisha yako ya kesho. Hapa ni lazima itafika mahali utatuliza sana akili yako ili kuweza ‘kuatamia’ kile kilichochema kwako.
Ukiona mtu mawazo yake yako hovyo hovyo na hajatulia kabisa, unapaswa kujua hata kesho yake haiwezi kuwa ya mafanikio itakuwa ni ya hovyo pia hivyo hivyo. Mawazo na hatua zako zinatakiwa kuwa makini sana kila wakati.
Ndio maana tunakwambia sana ni muhimu sana kuangalia matokeo haya ya kesho kabla hujatumia mawazo yako na kabla hujachukua hatua. Unatakiwa ujenge utamaduni wa kujiuliza mara mbil mbili kwamba je, hiki unachokiwaza kipo sahihi au la.
Amua kila wakati kupata matokeo unayoyataka kwa kuwa mwangalifu sana wa mawazo na matendo yako. Ukifanya uamuzi huo utakufanya uwe mshindi katika maisha yako kila wakati,  tofauti na ambavyo ungeacha mambo yaende tu kama yalivyo.
Kesho yako ya mafanikio makubwa, inajengwa na mawazo yako bora ya sasa, na pia inajengwa na matendo yako bora ya sasa, kwa namna yoyote ukishindwa kuangalia vitu hivyo matokeo yako ya kesho yatakuwa mabaya sana.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,















    

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.