google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 17, 2018

Achana Na Hadithi Zote Za Uongo, Njia Halisi Ya Mafanikio Yako Iko Hivi.

No comments :
Ili uweze kufika mahali fulani, kwa kawaida ipo njia ambayo inatumika ili iweze kukufikisha kule. Kwa mfano, kama upo Dodoma na unataka kwenda Kigoma ipo njia ambayo inatumika kuweza kukufikisha Kigoma na usizuiliwe na mtu kufika huko.
Hata katika safari yako ya mafanikio, ipo pia njia ambayo unatakiwa uifate na njia hiyo ikusaidie kukufikisha kule kwenye kilele cha mafanikio unako taka kufika. Njia hii ninayoiongelea ipo na ni kweli inakufikisha ukiamua iwe hivyo.
Lakini kwa bahati mbaya sana njia hiyo ya kuelekea kwenye mafanikio yako, si njia rafiki sana kwako, si njia ambayo imenyooka kama ulivyokuwa ukidanganywa au ukijidanganya wewe mwenyewe kipindi cha nyuma.
Njia hii ambayo unatakiwa kuifata hadi ikifukishe kwenye mafanikio yako ni njia ambayo ina mabonde, ni njia ambayo ina miinuko na pia ni njia ambayo ina miti na milima ya kila aina ambayo hukutegemea kama itakuwa hivyo.
Kwa kuwa najua umeamua kufata njia ya kukupeleka kwenye mafanikio yako, najua huwezi kukwepa kuifata njia hiyo ninayokwambia hapa. Ni jukumu lako kufata njia hii hadi iweze kukufikisha kule unakotaka kufika kimafanikio.

Ila kama hupendi kufika kule unakotaka kufika kimafanikio, naomba nikupe ruksa tu, unaweza ukaiacha njia hiyo na kuamua kufuata njia nyingine ambayo wewe mwenyewe kwako unaweza ukaona labda inafaa.
Kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa mvumilivu na kukabiliana na kila hali unapokuwa kwenye njia ya mafanikio. Ikiwa utaleta mchezo, utapata ajali na mwisho wake utafika kati na hutaweza kufanikiwa.
Kwa hiyo unatakiwa kuwa dereva mwangalifu, unatakiwa kuwa dereva mwangalifu kuangalia vikwazo au vizuizi vyote ambavyo vinaweza vikakukwamisha na ukashindwa kufika mwisho wa safari yako ya mafanikio.
Sina shaka unajua kiuwazi kabisa dereva yeyote anapokuwa barabarani anatakiwa kuwa makini sana, kama asipofanya hivyo ajali inaweza kumhusu. Hata wewe unapata njia ya kuelekea mafankio yako unatakiwa umakini huo uwe mkubwa sana.
Naelewa mpaka sasa umeshajua njia unayoifata inayokupeleka kwenye mafanikio yako si njia rafiki sana kwako yaani wakati wowote unaweza ukagonga mwamba au ukaingia shimoni kwa hiyo umakini unahitajika.
Nimekwambia haya kukuonyesha njia ya mafanikio unayaoifata jinsi ilivyo. Kama ulikuwa una hadithi zako kichwani kwamba njia unayoindea kwenye mafanikio ni njia iliyonyooka kama mstari mnyoofu, hapana hapo ulijidanganya.
Kuna mabonde na milima mingi sana au kwa lugha nyingine mafanikio hayapo kwenye mstari mnyoofu kama ambavyo unaweza ukadhani au ukafikiria. Ni jukumu lako wewe kuamua  kukomaa na njia hiyo mpaka kiweze kieleweka kwako.
Hata hivyo kama itafika wakati unaona njia hiyo ni ngumu kwako pia uamuzi ni wako kuamua kubaki pembeni na kuwaacha wengine wapite, huo ni uamuzi ambao unatakiwa kuuamua ipasavyo.
Ikiwa lakini utaamua kuchukua uamuzi wa kukaa pembeni na kuamua labda kutafuta njia ya mkato, hapo napo ndio naona unakuwa unajipoteza zaidi, maana mwendo huo unaweza ukawa ndiyo njia ndefu kuliko hata ile ya mwanzo ambayo ulikuwa unatakiwa uifate.
Ni nini ninachotakiwa kukwambia kupitia makala haya, ni kwamba unapaswa kuelewa mafanikio sio rahisi na njia ya kuelekea kwenye mafanikio yako sio rahisi pia. Kama njia ya kukufikisha kwenye mafanikio ingekuwa ni rahisi kila mtu angekuwa tajiri.
Unachotakiwa kufanya ni wewe kuwa mvumilvu, kuvumilia kila adha na ugumu unaokutana nao na hadi kuona mafanikio yako yanatokea. Ikiwa utakuwa unaona unaonewa kwamba wewe hukustahili kupata hayo unayokutana nayo utakosea.
Kila siku tafuta kitu cha kujifunza wakati upo kwenye njia ya mafanikio yako hata kama haieleweki, tafuta jinsi ya kuvuka vizuizi vyote na mwisho wa siku utajikuta upo kwenye ngazi kubwa sana  ya mafanikio kwako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.