google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 22, 2018

Haya Ndiyo Mambo Makubwa Mawili, Ambayo Ni Lazima Ukutane Nayo Sana Kwenye Safari Ya Mafaniko Yako.

No comments :
Katika safari yako ya mafanikio, yapo mambo makubwa mawili ambayo ni lazima ukutane nayo sana. Mambo haya kila binadamu anakutana nayo sana, hakuna mtu ambaye hakutani nayo hata kama hutaki mafanikio, utakutana nayo tu.
Hata kwa kila iitwapo leo, mambo haya pia utakutana nayo pia. Hakuna siku ambayo itapita bila kukutana na mambo haya mawili iwe kwa kidogo au sana utakutana nayo tu utake, usitake lakini uwe na uhakika utakutana nayo.
Mambo hayo ambayo kila mtu anakutana nayo kwenye safari ya mafanikio  ni fursa na changamoto. Kila mtu, kila siku anakutana na fursa na changamoto kwenye maisha yake. Hata leo ni lazima pia utakutana na mambo haya makubwa mawili.

kama nilivyosema, kitu cha kwanza ni fursa, kila kukicha zipo fursa ambazo utakutana nazo. Fursa hizi zinaweza zikawa zinaonekana kwa wazi au hazionekani kwa wazi. Hakuna haja ya kusema kwamba mbona mimi fursa hizo sizioni, sio kweli.
Kile kitendo cha kuamka tu na kukutana na watu na mkabadilishana mawazo, hiyo ni fursa kubwa sana kwako kwa siku. Kupitia watu hao mtabadilishana mawazo na wewe unaweza ukatapa kitu cha kuweza kukusaidia kwenye maisha yako.
Ikiwa lakini upo upo tu, unakutana na watu kazi yako nikupiga majungu na kujifanya wewe ndio mwongeaji sana, sahau hizo fursa kuweza kuziona. Utapotea sana na utabaki kila siku kulaumu kwamba dunia ngumu kwako kumbe sio kweli.
Kipi unachokiona kila kunapokucha? Unaona unazungukwa na fursa au unaona kila kitu unazungukwa na hasi nyingi ambazo haziwezi kukusaidia wewe maishani mwako. Unatakiwa kujifunza kutambua fursa za mafanikio yako kila siku.
Kitu cha pili ni changamoto, bila kujali unakutana na changamoto za ukubwa upi, lakini kila kukicha unakutana na changamoto. Na kupitia changamoto hizo ndizo zinatupaisha na kutufikisha kwenye mafanikio makubwa ikiwa utazitatua kwa kiasi kikubwa.
Angalia mafanikio yote duniani, yanapatikana kutokana na kutatua changamoto. Kwa jinsi unavyotatua changamoto, unazidi kujenga mafanikio makubwa sana maishani mwako kila siku.
Wapi ulipo, na wapi maisha yako yapo, hiyo haijalishi. Kikubwa tatua changamoto zinazokuzunguka na utaweza kufanikiwa. Huwezi kukwepa changamoto hata kidogo, changamoto za kimaisha zipo na ni lazzima ukutane nazo.
Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo makubwa mawili ambayo ni lazima uweze kukutana nayo sana kwenye maisha yako na kila siku. Jiandae kukutana na mambo hayo na ili yawe kwa faida kubwa kwako na ya kukufanikisha.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.