google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 21, 2018

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Anayetaka Usawa Sana Mwisho Wake Hugeuka Mchawi.

No comments :
Karibu rafiki na mpenzi msomaji wa mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO, sina shaka kwa wakati huu ni mzima wa afya na upo tayari katika siku ya leo kuweza kujifunza hekima za maisha na mafanikio kama ilivyo kawaida yetu. Naamini unaendelea kujifunza kupitia hapa jamvini na unapata kitu cha kukusaidia.
Kumbuka kama ninavyokwambia kila wakati, hekima za maisha na mafanikio zinakupa busara za maisha na mafanikio, zinakujengea misingi ya kimafanikio na hata uelewa wa kujua mambo kadhaa wa kadhaa kupitia babu zetu ama unaweza ukawaita wahenga wetu wa zamani, yote haya unayapata hapa ukiwa DIRA YA MAFANIKIO kila jumapili.
Sitaki nikuchoshe kwa maneno mengi sana, nikukaribishe tena jamvini tuweze kujifunza hekima za maisha na mafanikio za siku hii ya leo.

1. Anayetaka usawa  sana mwisho wake hugeuka mchawi.
Katika hekima hii ya maisha na mafanikio  ina maana kwamba, tukiwa sisi kama binadamu tukubali kuwa binadamu kutofautiana kupo. Siyo kwa sababu fulani kapata baiskeli ni lazima na wewe upate au fulani kapata nyumba na wewe unawaza  lazima nami nipate kwa njia yoyote hata isiyo ya halali.
Maneno kama haya mwishowe humsukuma mtu kutumia hila mbaya au njia zisizo za kawaida kama vile uchawi au kila aina ya dhuluma aijuae yeye ili kumwezesha kupata mafanikio hayo. Hekima hii hutumika sana  katika kuwaonya wanaopenda kujikweza na kujiona wao ni wao kwamba kila kitu lazima wapate kama wanavyowaona wengine.
Watu hao wanasahau kuwa si kila kitu mnaweza kuwa sawa. kujaribu kuwa sawa na watu wengine kwa kila kitu huko ni sawa na kutafuta kwako wewe kuweza kujiumiza. Kwa kuliona hili, hekima za maisha na mafanikio zimeweka wazi, ukitaka usawa mwisho wake hugeuka kuwa uchawi na huo ndio ukweli halisi hata kama unauma.
2.  Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha.
Kuna wakati unaweza ukawa unatenda jambo la aina fulani ambalo jambo hilo watu wengine wanakuwa hawalijui kabisa. Mtu huyu anayetenda jambo lisiilofamika katika hekima  anafananishwa na mtu mwenda usiku au mtu yule anayetembea usiku asijue ni nini kilichopo mbele yake ilimradi tu anaenda.  
Kwa kawaida mtu huyu anayetembea usiku au anayetenda jambo ambalo kwa wakati ule wengine hawalielewi na inapotokea jambo hilo linapoonyesha mafanikio ndipo watu wanaanza kumsifu. Hekima hii hutumika sana kwa mtu anayechekwa na wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati ule wale wamchekao hawaelewi usahihi wa lile alitendalo.
Si busara na si uungwana kuanza kumcheka mtu kwa kitu usichokijua hata kidogo na wakati mwenzio anakifanya. Kama ni kufanya mwache afanye, lakini ukiendelea kucheka yakitoka mafanikio jiandae kumsifia. Wapo watu ambao wanaonekana mashujaa baada ya kubezwa sana, ndio maana hekima zinatufundisha mwenda usiku amesifiwa kulipokucha.
Fanyia kazi hekima hizi na zikusaidie kuchukua hatua na kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,








No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.