google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 7, 2018

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maneno Hayana Mbawa, Lakini Yanaruka Umbali Mrefu Sana.

No comments :
Karibu rafiki, katika ukurasa huu wa hekima za maisha na mafanikio. Leo katika ukurasa wetu wa hekima za maisha na mafanikio sitakuwa na mengi sana, zaidi nikukaribishe ukaribie, tuweze kujifunza hekima za maisha na mafanikio kama ambavyo ilivyotolewa na wahenga wetu. Andaa kalamu yako na karibu mkekani tuweze kujifunza kwa pamoja;-
1. Mafanikio na uvivu ni vitu ambavyo havikai pamoja.
Ni hekima ambayo inatukumbusha kwamba uvivu na mafanikio ni vitu ambavyo haviwezi kukaa sehemu moja hata iweje. Hekima hii inaonesha ili uweze kufanikiwa ni unatakiwa uvivu kuweza kuuweka mbali bila ya kufanya hivyo, sahau kuweza kupata  mafanikio kwenye maisha yako.
Watu wengi utakuta ni watu wakutafuta mafanikio, lakini wakati huo huo ni watu ambao wanakuwa ni wavivu. Sasa maneno ya hekima za maisha ya mafanikio yanatukumbusha kwa uwazi mafanikio na uvivu ni vitu ambavyo haviwezi kukaa pamoja hata siku moja. Ni lazima uvivu ukae mbali mafanikio yatakuja.

2. Maneno hayana mbawa, lakini yanaruka umbali mrefu sana.
Kuna wakati unakuta habari inatoka hapa inaweza ikawa ya kweli au sio kwaeli, lakini baada ya muda mfupi habari hio utaikuta imezagaa eneo kubwa sana. Hiyo yote inaonyesha nini, kwamba maneno yana kasi kubwa ya kusambaa. Kasi yake ya maneno inayosambaaa inafananishwa na mbawa.
Pamoja na kwamba maneno hayana mbawa, lakini wahenga wanatukumbusha kwamba yanasambaa sana kama vile yamevishwa mbawa. Hapa ndipo tunapotadharuishwa na wahenga wetu kwamba ni muhimu kuwa makini sana na maneno yetu, vinginevyo habari zetu tutazikuta mbali sana.
3. Huweze kujua ulichonacho kama ni kizuri, mpaka umekipoteza.
Kwa kawaida kila mtu anathamani kubwa sana, thamani ambayo anatakiwa ajidai nayo kwa sabbu anayo. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui thamani kubwa walizonazo ndani mwao, mpaka thamani zile wanapoanza kuzipoteza ndio wanakuja kukumbuka kwamba thamani hizo wanazo.
Kupitia hekima na maisha na mafanikio, inatuonya na kutukumbusha ya kwamba, ni muhimu kutambua sana thamani ya vile vitu tulivyonavyo. Haijalishi ni kazi au kitu gani. Lakini ukishajua thamani ya ulichonacho na ukakitunza kwa ufasaha hiyo itakusaidia  hata kuweza kupata na vitu vingine. Jua thamani ya ulichonacho na ikutunze.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.