google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 18, 2018

Hamasa Nne Za Ushindi Wa Mafanikio Yako.

No comments :
Mbali na malengo unayojiwekea, maisha ya mafanikio yanahitaji sana pia hamasa na msukumo utakaokusaidia wewe kuweza kusonga mbele kila siku. Pasipo kuwa na msukumo au mhemuko huo hakuna hatua kubwa utakazoweza kuchukua.
Ndio maana ni muhimu kuwa na hamasa au kitu kinachokufanya uchukue hatua kila siku. Kwa sababu hiyo ndiyo maana kila siku unajifunza hapa ili kupata maarifa ya kukusaidia kusonga mbele na hamasa pia. 
Kama nilivyosema Unatakiwa ujifunze kila siku na kupitia kujifunza ndio unajikuta unahamasika pia kuchukua hatua. Leo kupitia makala haya naomaba tujifunza hamasa nne muhimu za kukusaidia kukupa mafanikio maishani mwako.

HAMASA YA 1, Muda wa mafanikio.
Jipe muda wa kufanikiwa kwa kuamua kutumia muda wako vizuri. Ukijipa muda wa kufanikiwa halafu wakati huo huo ukawa mvumilivu na king’ang’anizi utafanikiwa.
Kitu kimojawapo kinachokufanya ushindwe kufanikiwa ni kwa wewe kushindwa kujipa muda wa kufanikiwa na kuamua kukata tamaa mapema.
Tumia muda wako vizuri kwa kila dakika unayoipata muda huo utakupa mafanikio yako, kuliko kuupoteza bila sababu za msingi.
Kama nilivyosema, jenga uvumilivu na amua kuwa king’ang’anizi ili kujipa muda wako sahihi wa mafanikio.
HAMASA YA 2, Kuwa mtu wa muhimu.
Amua kuwa mtu wa muhimu, amua kuwa mtu wa thamani. Kwa jinsi unavyoendelea kuwa mtu wa muhimu na mtu wa thamani hivyo ndivyo ambavyo utazidi kupata mafanikio katika dunia hii.
Mafanikio uliyonayo yanatoa picha ni kwa jinsi gani ambavyo wewe thamani yako ilivyo. Kama una mafanikio kidogo basi ujue kabisa hata thamani unayoitoa na umuhimu wako ni kidogo pia bado.
Hivyo unapaswa kubadilika mara moja na kujua thamani bora ambayo utakuwa unatoa hiyo ndio itakayokuwa inakupa na sio vinginevyo. Anza leo kukuza thamani na umuhimu wako ili uvune mafanikio yako.
HAMASA YA 3, Juhudi na mafanikio.
Kama hutaki kuweka juhudi kubwa kwa kile unachokifanya, basi jiandae kupata matokeo sawa sawa na juhudi zako hizo unazoziweka. Huwezi kupata matokeo kinyume na juhudi unazoziweka hata siku moja, ni lazima utapata matokeo yanayoendana na juhudi zako hizo unazoziweka.
Kwa hiyo ni swala la wewe kuangalia, unaweka juhudi za aina gani kwenye kile unachokifanya. Juhudi zako hizo ndizo zitakazoamua zikupe matokeo ya aina gani. Kama unaweka juhudi kubwa utapata matokeo makubwa, kama unaweka juhudi kidogo basi utapata matokeo kidogo, kusiwe na mtu wa kumlaumu tena kwako.
HAMASA YA 4, Matokeo ya juhudi zako.
Mafanikio uliyonayo mpaka sasa, ni matokeo ya juhudi na nguvu zako ulizojitoa ndizo zilizokufikisha mpaka hapo sasa ulipo. Mafanikio hayo uliyonayo, hujayapata kwa bahati mbaya ni matokeo ya kujitoa kwako kwa namna fulani hivi.
Pasipo kuangalia una mafanikio ya aina gani, lakini ni matokeo ya kujitoa kwako. Kama ulijitoa kidogo basi tunaona mafanikio yako ni kidogo pia, kama umejitoa kwa nguvu zote na juhudi zote basi ni wazi tunaona mafanikio makubwa pia.
Ni nini unachotakiwa kufanya kama huridhishwi na mafanikio yako? hakuna kingine zaidi ni kuongeza ile nguvu ya kujitoa. Endelea kujitoa zaidi na zaidi, endelea kutafuta maarifa zaidi, endelea kuongeza juhudi utapata mafanikio makubwa.
Hakuna ambaye anayeongeza juhudi na kuamua kujifunza halafu akaangushwa. Mtu huyo hayupo. Chukua hatua leo ya kuendelea kuweka juhudi za ziada kwa kila ukifanyacho ili juhudi hizo zikufikishe kwenye mafanikio uyatakayo.
Fanyia kaza haya, na chukua hatua sahihi za kuweza kufikia ndoto yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.