google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 23, 2018

Fanya Jambo Hili Tu, Pale Unapoona Maisha Yako Hayaeleweki.

No comments :
Inapotokea pale unaona maisha yako yanakuwa magumu sana na unaona kama ulimwengu wote unakusaliti kitu pekee ambacho unatakiwa ukifanye kwa wakati huo jiweke bize, fanya kitu kitakacho kushughulisha sana kwa siku nzima.
Inapotokea tena  unaona huna kitu mfukoni mwako na unajiona wewe ndio maskini wa kutupwa, amua kujiweka bize kwa kwa kufanya kazi kwa bidii sana, tafuta kitu kitakachokupa changamoto na kukutoa hapo ulipo.
Inapotokea wewe unajiona ni mtu wa kuonewa na kutaka kulalamika sana, futa kwenye akili yako kuonewa huko. Kitu cha kufanya anza kujiweka bize kwa mambo yako na kuonewa huko ambako unafikiri hautakuona tena zaidi utaona amani tu kwako.

Inapotokea kwenye maisha yako umejawa na woga na hofu hadi kufika mahali huoni tumaini lolote mbele yako, tena kitu cha kufanya hapo ni kujishughulisha na kuwa bize zaidi kila wakati kwenye maisha yako.
Zipo nyakati nyingi ngumu ambazo zinakuwa zinatutokea kama hizi ambazo nyakati hizo hufungua milango ya kutaka kutufanya sisi tuyaone maisha yetu ni magumu na tumechelewa sana. Unatakiwa kujua inapotokea hali kama hii kumbuka kuwa bize.
Unapokuwa bize ni dawa pekee ambayo inakusaidia wewe kusahau kila kitu na mwisho wa siku unajikuta ndoto zako zimetimia mapema sana kuliko unavyoweza kufikiria hapo awali. Hivyo kujishughulisha ni kitu cha msingi sana kwako.
Pale unapokuwa bize na kufanya mambo yako, pia inakusaidia kuweza kuona fursa nyingine zaidi. Kwa tahadhari hapo,  kuwa bize kwa yale mambo ya msingi tu, usiwe bize kwa mambo ambayo hayawezi kukupa faida kwako.
Ukweli na uhalisia ambao naweza kukupa katika maisha ndio huo. Unajiwekea mikakati ya kushughulisha hata kama inatokea hali gani kwako, wewe jiweke bize hiyo ni dawa kubwa sana kwako ya kuweza kukufanya uweze kusonga mbele kwenye maisha yako.
Kuanzia sasa amua kujishughulisha sana kwenye mambo yako. Usikubali muda upite hivi. Kama utajishulisha kila wakati kwanza hiyo itakupa mafanikio, pia si hivyo tu inakusaidia kuweza kupata fursa na mafanikio mengine kwako.
Ndio maana tumekwambia pale unapoona maisha hayaeleweki, yamekuwa kama ya hovyo sana, ni jukumu lako kuwa bize ili usiweze kukaribisha msongo wa mawazo na mawazo yasiyo na maana kwako tena.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.