google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 11, 2018

Zijue Kanuni Bora Za Mafanikio Yako Kwa Mwaka 2018.

No comments :
U hali mpenzi msomaji wetu wa mtando huu wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka u mzima na unaendela vyema na majukumu yako ya kila siku.

Kama ulivyo msemo, usemao kizuri kula na wenzako basi nami bila hiana nakukaribisha jamvini ili tule kwa pamoja chakula kinachoitwakanuni za mafanikio kwa mwaka 2018”.

Naomba utambue ni chakula ambacho hakina madhara yeyote katika afya yako, lakini pili chakula hiki pindi utakapokula kitakupa mwangaza mpya wa maisha yako. Nimeona nikwambie mapema faida ya chakula hiki ili usije ukasema umeshiba.

Miongoni mwa kanuni muhimu ambazo unatakiwa kuzifahamu katika mwaka huu ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni kama ifuatavyo;


1.    Elimu.

Kila kitu ambacho unakiona katika dunia hii, ipo misingi mikuu ya elimu hadi kitu hicho kimeweza kufanikiwa. Hatuzungumzii elimu ya darasani pekee, la hasha zipo elimu nyingine ambazo hazikuitaji uiingie darasani  bali unaweza kujifunza kutoka sehemu tofauti tofauti mbali na kukaa darasani.

Elimu hii unaweza kujifunza kwa watu ambao tayari wamekwisha fanikiwa au katika vyazo mbalimbali vya utoaji elimu kama vile makongamono, warsha,vitabu na katika mitandao ya kijamii.

Hivyo ili uweze kuwa bora katika maisha yako ya kila siku hasa katika mwaka huu 2018, ni vyema ukawekeza muda mwingi katika kujifunza katika jambo hilo. Kwani ukweli ambao upo bayana kwa wote waliofanikiwa ni kwamba watu hao wamewekeza muda mwingi katika kujifunza, na kujifunza huku hakikisha hakuna ukomo.

2.   Hamasa.

Jambo la pili ili uweze kufanikiwa zaidi katika mwaka huu ni vyema ukahakiisha ya kwamba unakuwa na hamasa ya kuweza kufanikiwa zaidi, na hamasa hii itokane na njaa ya kufanikiwa, hivyo kila wakati ni lazima utafute kitu ambacho kitakupa motisha ya kuweza kufanikiwa ziaidi.

Na miongoni mwa vitu hivyo kwanza hakikisha unazungukwa na marafiki sahihi lakini pili hakikisha ya kwamba kwa jambo lolote ambalo unalifanya unakuwa unalipenda.

3.   Kutenda jambo hilo.

Mara baada ya kupata elimu, hamasa jambo linalofuata ni kutenda jambo hilo. Mara nyingi watu wengi  huwa wanapata elimu na hamasa tu, jambo ambalo linafanya watu hao waweze kukomea kwenye hatua hizo mbili tu. Ila kwa kuwa wewe ni msaka mafanikio na unataka kufanikiwa zaidi ni vyema ukahakiisha ya kwamba unafika mpaka hatua ya tatu ya kulitenda jambo hilo, na katika kulitenda jambo hilo ni hakikisha unalitenda kwa juhudi zote ulizonazo.

Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba kanuni ambazo zitakusaidia wewe uweze kufanikiwa katika maisha yako ni ELIMU+HAMASA+KUTENDA=MAFANIKIO.

Ndimi Afisa Mipango Na Mafanikio Benson Chonya
07576-909942.



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.