google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 4, 2018

Kile Kitachokufanikisha Mwaka 2018 Ni Hiki.

No comments :
Kuna wakati tunajiambia sana ‘mwaka huu nahitaji kuongeza mtaji, mwaka huu nahitaji pia kufanya biashara ile, au mwaka huu nahitaji kufanya hiki au kile’. Hizi ni sentensi ambazo naamini umezisikia sana zikisemwa na kuna kipindi hata wewe umekuwa ukijisemea hivyo.
Katika ulimwengu wa mafanikio ipo hivi kile kinachokufanikisha si kile unachokihitaji, bali kile kinachokufanikisha ni kile unachokifanya au kukifanyia kazi, ndicho hicho kinachokufanikisha na kukupa mafanikio.
Hakuna atakayejali kwa kile unachohitaji au unakisema sana hata kiwe kizuri vipi, dunia inajali kile unachokichukulia hatua na kukifanya. Hicho unachokifanya kila siku, hicho ndicho kinachokusogeza kwenye mafanikio yako.

Unaweza ukahitaji mambo mengi sana lakini kama huchukui hatua uwe na uhakika huwezi kufanikisha kitu chochote katka maisha yako, zaidi yako utaishia kusema nahitaji hiki au kile na miaka inaenda na bado ukajikuta hupati kitu.
Kuna watu ambao ukiwachunguza karibu maisha yao yote ni watu wa kusema nitafanya hiki mwaka huu au kile na hawafanyi. Maisha ya mafanikio hayataki ‘blaa blaa’ yanataka ufanye kitu yaani uchukue hatua za kimafanikio.
Unachotakiwa kuhakikisha ni kwamba mwaka 2018, uwe mwaka ambao usiweke maneno sana. unatakiwa kuchukua hatua kwani kile kinachokufanikisha ni kile ambacho unakifanyia kazi na si kile unachokisema tu.
Unaweza ukasema mengi sana na inawezekana tayari umeshasema mpaka sasa hivi, kitu unachotakiwa kujiuliza je, vitu hivyo unavichukulia hatua au huchukui hatua yotote ile ya kuweza kukusaidia kufanikiwa?
Kumbuka unachokihitaji hakiwezi kukupa mafanikio unayoyataka kwa asilimia zote, acha kulinga na kujidai kwa kile tu unachokihitaji, badala yake uelewe kabisa kile unachokifanya hicho ndicho kitakachokupa maisha na mafanikio unayotaka.
Hatua kwa namna yoyote ile inahitajika sana ili kuweza kufanikiwa kwako. Unatakiwa kuelewa pasipo hatua yoyote au utendaji sahau kabisa mafanikio kwa mwaka 2018, zaidi utaendelea kuzunguka tu na kuwa wewe kama yule wa miaka iliyopita.
Kitu cha msingi cha kuondoka nacho hapa leo ni kwamba, kile kitakachokufanikisha kwa mwaka 2018 ni kile tu ambacho utakichulkulia hatua lakini si kinyume cha hapo. Kwa hiyo, ni lazima sana kwako kuweza kuchukua hatua ili kufanikiwa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.