google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 13, 2018

Mbinu Za Masoko Kwa Wafugaji.

No comments :
Habari  rafiki, leo nimependa kuzungumzia swala la masoko ya mazao ya ufugaji kama unavyojua tunafuga na mwisho wa siku lazima tuingize mazao yetu sokoni, kumekuwa na changamoto kubwa kwa wafugaji wengi katika kupeleka mazao yao ya mifugo sokoni.

Wengi wananipigia simu wananiambia wanamazao ya mifugo lakini hawajui wapi watauza kuku wao wengine wananiambia wana mayai hawajui watawauzia wapi hii imekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi.

Leo nimeona nije na mbinu au kanuni ambayo inanisaidia mimi na huwa inawasaidia watu wengi pia katika kufanya biashara zao za kuku na mwisho wa sikui na wamekuwa wanafurahi sana kwasababu soko ni kubwa na mafanikio ni makubwa.

Wewe ambaye umeingia katika uwekezaji huu wa kuku na umekuwa ukihangaika kupata wateja wa mazao yako ya ufugaji karibu sana katika somo hili la leo uweze kujifunza na kufurahia ufugaji wako.


 MIGHAHAWA MIKUBWA NA MIDOGO.

Hii ni sehemu nzuri sana ambapo unaweza kufanya biashara yako ya mazao ya ufugaji (kuku na mayai), hawa ni watu ambao wanauhitaji mkubwa wa kuku na mayai kwa ajili ya chakula cha biashara katika biashara zao.

Nimekuwa nikifanya nao biashara mara kwa mara sehemu hii na wamekuwa wateja wangu wakubwa na bei zao ni nzuri sana, wao mara nyingi wanapelekewa kuku na mayai na madalali sasa wewe kama mfugaji ukitembelea sehemu hii utafanya biashara nzuri sana. 

WAUZAJI WA SUPU.

Hawa utawakuta maeneo mengi ya mijini hasa maeneo ya stand, baa, soko, hospital, utawakuta wanauza supu hawa niwateja wazuri sana wa kuku mimi mwenyewe nishahidi mzuri sana wa hili.

Kwa mfano hapa nilipo kuna watu wamenizunguka wanafanya biashara ya supu nashuhudia wakihangaika kutafuta kuku hadi wanaenda sokoni kutafuta kuku, sasa huoni wewe unahangaika bure wakati soko unalala nalo nyumbani sasa wewe endelea kulalamika sisi tunakuacha.

WATU WENYE MASHEREHE.

Eeeh! yaani hadi hapa utaniambia soko hakuna rafiki changamka ufugaji wako ni Pesa yako, ulizia wapi kunasherehe mwezi huu katika mtaa wako hata wilaya yako kawaambie mimi nitawauzia kuku mkihitaji utashangaa watakavyochangamkia fursa, nenda kaonane nao utaniambia.

Nimekuwa nashuhudia watu wanaweka sherehe kuku wanapita kutafuta mitaani na kwenye vibanda vya kuku ili wapate kuku kwanini wewe usiwarahisishie kazi kwa kuwaambia utawapelekea kuku, endelea kushangaa na kufa njaa wakati chakula unacho mimi sipooo!

FUNGUA VIBANDA VYA KUUZA KUKU.

Nimekuwa nikishudia watu wengi wakihitaji kuku na hawajuwi wapi watapata wananiambilia sehemu zenye vibanda vya kuuzia kuku ili kujipatia kuku, cha kushangaza vibanda vingi havimilikiwi na wafugaji Bali vinamilikiwa na wafanyabiasha.

Sasa wewe unaonaje ufungue kibanda chako na unakua unauza kuku hapo, kiukweli sijui na wala siamini kama kunachangamoto katika soko la kuku kwa maana naliona pana sana.

MADUKA YA MATUMIZI YA NYUMBANI.

Hapa ni sehemu ambayo watu wengi huwa tunaenda kununua matumizi mbalimbali ya nyumbani sehemu nyingi huwa kunakuwa na mayai wanauza wewe unadhani wanafuga wao wenyewee! Hapana wananunua sasa unaonaje kama wewe ukiwa mmoja ya watu wanaowapelekea mayai.

Sasa wewe kaa hivyo hivyo na kusema ufugaji hauna soko na ujihakikishie kufeli kwenye ufugaji mimi sipo wewe baki ukilia peke yako mimi masoko ninayo yakutoshaaa!

TUMIA KUNUNI HII ILI UNASE WATEJA WA KUTOSHA

Nenda stationary  katengeneza business card ambayo utaandika taarifa zako muhimu na  mazao ambayo unayo nyumbani kama vile (kuku na mayai) baada ya kutengeneza kadi yako ya biashara nenda maeneo ya kazi mfano: maofisini (bank, hospital, shuleni, na sehemu mbalimbali za ofisi).

Ukifika maeneo hayo zungumza nao kwa uchache kwa sababu wapo maeneo ya kazi hawaweze kukaa kukusikiliza wewe hivyo unachotakiwa kufanya  wagawie kadi yako ya biashara na waambie wakutafute  nakuhakikishia utapokea wateja hadi utashangaa, naomba nikwambie unadhani wafanyakazi wakiwa na shida na nyama au mayai nani atakuwa wakwanza kutafutwa kama siyo wewe, sasa wewe shangaa watu tubebe wateja wako.

Hizi ni baadhi tu ya masoko kuna mengi sijayazungumzia fanyia kazi hayo kama kuna sehemu utafeli karibu tuzungumze.

Ni Mimi rafiki yako 
Frank Mapunda,
Mawasiliano yangu ni
0758918243/0656918243



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.