google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 5, 2018

Mambo 10 Unayotakiwa Kuyazingatia Na Kuyasimamia Mwaka 2018.

No comments :
Yapo mambo mengi sana ya msingi ambayo unapaswa kuyazingatia kila siku katika safari yako ya mafanikio. Kwa bahati nzuri mambo hayo tumekuwa tukiyaeleza sana hapa DIRA YA MAFANIKIO karibu kila siku.
Katika mwaka 2018 kitu cha muhimu au mambo muhimu ambayo unatakiwa kuyazingatia na kutembea nayo ni kama haya yafuatayo;-
1. Unapofika wakati tayari umeshaamua kufanya kitu fulani, anza kukifanya kitu hicho mara moja, acha kuchelewa sana.  Kwa mwanzo hata kama unaona mambo ni magumu na hayaeleweki, ukilazimisha kuanza, mwisho wa siku mambo hayo kadri unavyoyafanya utazidi kupata uzoefu na kujikuta ukizidi kusonga mbele kimafanikio.
2. Kuwa na mawazo bora sio ndio mafanikio tayari bali ni njia ya kukufikisha kwenye mafanikio ikiwa utachukua hatua sahihi. Hivyo acha kujisifu una mawazo bora na kujiona umefanikiwa tayari, wazo bora ni sawa na barabara inayokuongoza kwenye safari yako. Mawazo bora ukiongeza na vitendo ndio sawa na MAFANIKIO.
3. Kuwa makini sana na yale yanayoitwa matumizi ya hovyo na madogo madogo. Matumizi hayo madogo madogo ndiyo yanayopelekea wewe kupoteza pesa nyigi sana ambazo kwa baadae zingeweza kukusaidia.

4. Kuna wakati unaweza ukawa ni chanzo cha kushindwa kwako kwa sababu ya kushindwa tu kuweka juhudi zinazotakiwa kwa kile unachokifanya. Ili kufanikiwa unatakiwa kuweka juhudi kubwa sana zitakazokusaidia kuweza kufanikiwa.
5. Kufikia mafanikio makubwa, inakutaka na wewe uwe mtu wa tofauti. Inatakiwa kufanya vitu vya tofauti na kuishi kwa tofauti, hapo utaweza kumudu kutatua matatizo makubwa ya watu na wewe ukawa mshindi katika maisha yako. Haiatawezekanai kufanikiwa na kufika juu kabisa, kama utaendelea kubakia kama ulivyo.
6. Inawezekana umefanya kosa wewe au kosa hilo limefanywa na mtu mwingine. Lakini kama ni kosa tayari limeshafanyika. Kama kuna kosa tayari umeshalifanya haina haja ya kujuta sana, unatakiwa kuachana na kosa hilo na kuamua kusonga mbele. Nguvu zako elekeza mbele kwa ajili ya kesho na achana na kufikiri kosa ambalo limeshatokea na huwezi kurudi nyuma tena kulirekebisha.
7. Upo ulazima wa wewe kufanya mambo ambayo wakati mwingine unafikiri huwezi kufanya. Unapofanya mambo hayo yanakupa ukomavu mkubwa wa kuweza kufanya mambo mengine zaidi na zaidi. Kama hauko tyari kufanya mambo amabayo kuna wakati unafikiri huwezi kuyafanya, kupiga kwako hatua, kitakuwa ni kutakuwa kwa tabu.
8. Tenga jumapili moja kila wiki, halafu tafuta muda ambapo kila jioni unakuwa unakaa angalau saa moja na kuanza kutafakari juu ya maisha yako wapi unapotoka na wapi unapokwenda na kisha kupanga mipango ya wiki linalofuata. Tabia hii ukiisimamia kiuhakika, itakufanya upige hatua sana.
9. Kaa karibu na watu ambao utaamua kujifunza vitu kutoka kwao. Usikae na watu ambao wanaweza kukuzamisha kimaisha, watu hao ni hatari sana kwenye maisha yako kimafanikio na ni rahisi kukurudisha nyuma.
10. Usiende kitandani kulala ukiwa na kazi yoyote ya kufanya au kuna jambo la kina la kulifikiria. Kitandani pako pafanye iwe ndio sehemu ya wewe kwenda kupumzika, ukienda kulala, na ulale kweli kama mtoto mdogo mdogo.
Naamini kwa kujifunza mambo hayo, itakusaidia sana kuweza kupiga hatua na kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.